Wateja
wa Skylight Band wiki iliyopita walipata nafasi ya kuburudika na
kinywaji kipya kabisa toka nchini Sweden MOKAI Cult ambacho kina Alcohol
4.5 yenye ladha murua kama aina ya Savanna ambacho ni zaidi ya Savanna.
Hakika
wateja wa Skylight Band katika ukumbi wa Thai village Masaki wiki
iliyopita walichangamka kweli na kinywaji hiki toka huko Sweden chenye
Alchohol ya wastani ambayo mtu anaweza kumudu kunywa na kuamka safi
kabisa bila Hang-Over.
Mashabiki wa Skylight Band wakiingia getini walipata fursa ya kuonjeshwa kinywaji hicho kipya kutoka Sweden kinachotambulika kama MOKAI Cult ambacho kitakuwepo kila siku ya Ijumaa ndani ya Thai Village jijini Dar na kuzidi kuwachangamsha mashabiki wa Bendi hiyo kusakata Rhumba zaidi.
Mrembo wa MOKAI Cult akifafanua jambo kwa wateja juu ya kinywaji hicho kipya.
Mbunifu wa Mavazi Gabriel Mollel akiuza sura na Models Neema Mbuya pamoja na Anna.
Miss Tanzania 2011 Salha Israel (wa tatu kulia) kwenye picha ya pamoja na marafiki zake ndani ya Thai Village-Masaki jijini Dar Juma lililopita.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakipata Ukodak na Warembo wa MOKAI Cult waliokuwa wakaribu kwa wateja na kutoa huduma yenye kiwango cha kimataifa. Njoo wewe na yule leo tujikoki na MOKAI.
Rappa wa Skylight Band Joniko Flower akiongoza makamuzi na kikosi kazi cha band hiyo kutoa burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village jijini Dar.
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Aneth Kushaba AK47 katika burudani ya aina yake yenye kiwango cha kimataifa kwa mashabiki wake.
Picha zaidi: MO BLOG
0 comments:
Post a Comment