Pichani juu na chini ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi za Zanaki, Diamond, Kisutu na Muhimbili katika siku maalum inayotambulika kama "Fun Thursday" na kufanyika Alhamis ya mwisho wa mwezi.
Bi. Ledama ametumia siku hiyo kuwaelimisha wanafunzi kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yakiwemo Malengo ya Milenia ambayo ni Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, Elimu ya Msingi kwa wote, Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wanawake, kupunguza vifo vya watoto wachanga, Upatikanaji wa huduma bora za uzazi, kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine, kulinda mazingira pamoja na kujenga mshikamano wa kimaendeleo duniani. Fun Thursday imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za UNESCO jijini Dar leo.
Wanafunzi wakimsiliza kwa umakini wakati Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) wakati akiwapiga msasa kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Msaidizi wa Maktaba ya kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na Maktaba mashuleni mwao pamoja na kujijengea tabia za kupenda kujisomea.
Wanafunzi wakifurahi wakati wa Fun Thursday inayofanyika kila Alhamis ya mwisho wa mwezi na kuratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
Mwalimu Nicholaus Massawe wa shule ya msingi Zanaki akibadilishana mawazo na Mwalimu Rahel Fute wa Shule ya msingi Diamond wakati wa Fun Thursday iliyowakutanisha wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali za jijini Dar.
Mratibu wa Mkoa kutoka Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Innocent Mkota akiwasisitiza wanafunzi umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa mashuleni.
Wanafunzi wa shule za mbalimbali za msingi jijini Dar es Salaam wakifuatilia Documentary fupi iliyomshirkisha msaani wa muziki wa Marekani Beyonce na wimbo wake wa "I was here" inayoenyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa Duniani.
Mwalimu Kalabo Mushumbusi kutoka shule ya Msingi Muhimbili akitoa shukrani kwa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC kuwa kuwaelimisha wanafunzi wao kuhusiana na kazi mbalimbali ya Umoja Mataifa nchini.
Wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) pamoja na walimu wao nje ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi za UNESCO.
0 comments:
Post a Comment