Mbunge wa Same Mashariki (CCM) Anne Kilango Malecela amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kuacha kukaa vikao vya majungu na kuwasema watu na badala yake wakatumie muda huo kufanya kazi.
"Mheshimiwa Spika naomba leo niseme kuwa, wabunge kila mmoja wetu tukae chini na kujiuliza iwapo tunafanya kazi ya wapiga kura wetu ambao wametuingiza madarakani,"alisema Kilango.
Anne Kilango aliyasema hayo jioni hii wakati akichangia Mpango wa maendeleo wa Serikali kwa miaka 5 uliokuwa ukijadiliwa Bunge mjini Dodoma.
Mbunge huyo ameomba wabunge kuchukua vitabu vyao vya dini na kukaa na kutafakari ni nini wamewafanyia wananchi wao japo kwa siku nzima tu na kuacha majungu na vikao vya kujadili namna ya kuondoana madarakani ilhali kazi hiyo ni yawananchi.
Aidha katika hilo amewaomba wananchi kuangalia upya Wabunge wao waliowachagua kama wanafanya kile walicho watuma na vinginevyo wasiwapigie kura tena ya kuwarejesha bungeni humo.
"Wananchi angalieni...mtu asiyefaa haina haja ya kumrudisha tena bungeni hapa, muondoeni," alisema Kilango.
Baada ya kuketi Spika wa Bunge Anna Makinda alisifu kauli ya Bunge huyo na kusema kuwa hiyo ni njia sahihi ya kujikosoa na ni kweli baadhi ya wabunge huacha kufanya yaliyo muhimu na kufanya mambo yasiy stahili.
0 comments:
Post a Comment