Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2013

Baadhi ya wanafamilia ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Isaack Mruma wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa marehemu Jerri Isaack Mruma ambaye ni Mtoto wa Mhariri Mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Isaack Mruma aliyefariki hivi karibuni jijini Nairobi Kenya kwa kunyongwa na watu wasio julikana. 

Mwili wa Jerry umewasili nchini leo na ndege ya shirika la Kenya Airways na anataraji kuzikwa kesho mchana makaburi ya Kinondoni baada ya ibada itakayo fanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach.
 
 Watoto wa Isaack Mruma, Kelvin Mruma (kulia) na kakayake Khan Mruma  wakipeana faraja pamoja na mwanafamilia mwenzao wakati wa kusubiri mwili wa ndugu yao.
Baadhi ya wanafamilia.
 Wafanyakazi mbalimbali wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakiwa uwanjani hapo wenye majonzi.
Wanafamnilia wakifanya mawasiliano walipofika uwanjani kuupokea mwili.
 Wafanyakazi wa TSN.
 Kaimu Mhariri Mtendani wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mwananchi Comunication, Tido Mhando uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo wakati wa kuupokea mwili wa Jerry Mruma mtoto wa Mhariri Mtendaji wa zamani wa TSN.
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) ambako Isaack Mruma alikuwa akifanya kazi kama Mhariri Mtendani, Gabriel Nderumaki (kulia) akimfariji Mruma kufuatia msiba wa kijana wake Jerry Mruma akliyefariki kwa kuuwa nchini Kenya.
Isaack Mruma akifarijiwa na mmoja wa watoto wake Kelvin Mruma uwanjani hapo mara baada ya kuupokea mwili wa Jerry.
Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Joseph Kulangwa(kulia) akimfariji Isaack Mruma kutokana na msiba huo wa mwanae.
 Mkurugenzi wa Mwananchi Comunication, Tido Mhando akimfariji Isaack Mruma.
Posted by MROKI On Monday, November 25, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo