Nafasi Ya Matangazo

November 22, 2013

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung  mjini Zanzibar.

Na Francis Dande
WARATIBU wa Tamasha la Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions ya Jijini Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza wamesema kuwa watapeleka uhondo wa tamasha hilo katika mji wa Zanzibar. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kutikisa kwa mara ya kwanza katika mji wa Zanzibar, Alex Msama alisema kuwa mbali ya Zanzibar, mkoa mwingine ambao umeongezeka ni Tanga.

Msama aliwataka wakazi wa Zanzibar na vitongoji vyake kuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha, hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa  Mao Tse Tung, ambapo sehemu ya fedha zitapelekwa katika kusaidia kuwalipia ada watoto yatima wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Hivyo, Msama aliwataka Wazanzibar kufika kwa wingi katika tamasha hilo ili kufanikisha malengo hayo, kama alivosisitiza kwa wakasi wa mikoa yote ambayo tamasha hilo litarindima.

Katika kufanikisha mpango huo, Msama ambaye ni Mkurugenzi pia wa Msama Promotions, ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki, wadau na wapendwa katika Kristo Yesu, wajitahidi kumuunga mkono kwa kufika kwenye Tamasha hilo litakalozinduliwa rasmi Desemba 25 jijini Dar es Salaa, kisha kufanyika katika mikoa saba.

Alisema baada ya Dar es Salaam, litahamia mkoani Morogoro Desema 26 kabla ya kwenda Moshi, Desemba 28 kisha kuvamia jiji la Arusha  Desemba 29, na mjini Dodoma, mikoa mingine ni Tabora, Tanga, Mbeya na Mwanza.

Alisema mbali ya malengo mengine, pia tamasha la hilo litakuwa na ujumbe wa kuhimiza amani  nchini chini ya kaulimbiu ya ‘Tuilinde na Kuidumisha Amani Yetu.’

Kwa upande wa waimbaji watakaopamba tamasha hilo la kimataifa, ni kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na wenyeji Tanzania.

Msama alisema kuwa maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yanakwenda vizuri na kuwataka watu wajitoleze kwa wingi kupata ujumbe wa Neno la Mungu kwa njia ya sauti za waimbaji mahiri waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia hiyo. 
Posted by MROKI On Friday, November 22, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo