Nafasi Ya Matangazo

November 28, 2013

Meneja wa Smile Tanzania na Uganda Fiona McGloin  (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha leo. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mtandao, Madaha Francis na Mkuu wa Mauzo, Deo Ndejembi.
Leo, Smile Communications Tanzania (Smile) inazindua huduma zake za Fourth Generation Long Term Evolution (4G LTE) mkoani Arusha, ikileta mapinduzi ya intaneti yenye kasi kwa wafanyabiashara, mashirika na wakazi wa ndani na wanaozunguka jiji la Arusha.
Smile inatoa intaneti yenye kasi zaidi katika soko; mtandao wake 4G LTE hutoa huduma za intaneti kwa kasi ambayo watoa huduma wengine hawawezi kuifikia. Mtandao wa Smile hutumia teknolojia ya mawasiliano iliyoendelea zaidi na viwango vya ubora vinavyoendana na sehemu nyingine duniani, na hutoa kasi isiyo na mpinzani, uhakika, ubora na urahisi wa matumizi ambao huboresha matumizi ya mtandao.
LTE (Long Term Evolution) ambayo pia inajulikana kama 4G LTE inawezesha upatikanaji wa intaneti yenye kasi zaidi kwa sababu ndiyo kiwango cha teknolojia cha kisasa cha kizazi cha nne (fourth generation – 4G) na inawakilisha mabadiliko ya hatua katika mageuzi kutoka kwenye teknolojia zilizopo za mawasiliano bila waya (wireless) kama vile GSM- 2G/GPRS/EDGE na UMTS-3G/3.75G. 4G LTE ni kizazi kipya cha mtandao pamoja na mawasiliano ya sauti na intaneti, na muundo wake unaoweza kubadilika na kuboreshwa mara kwa mara, una hakikisha kuwa 4G LTE itabaki kuwa kiwango bora zaidi cha huduma za intaneti na sauti kwa miaka ijayo.
"Smile ilizinduliwa jijini Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2013, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mapinduzi haya ya kiteknolojia. Tuna furaha kubwa kuwaletea huduma hii jijini Arusha. Kama kitovu mashuhuri kimataifa ambacho kina sekta iliyo kubwa, inayokua kwa kasi na yenye nguvu zaidi katika huduma za utalii na taasisi mbalimbali za elimu, Arusha ina biashara nyingi, mashirika na watu ambao watafaidika kutokana na huduma zenye intaneti yenye kasi, "alisema Fiona McGloin , Meneja wa Smile Tanzania na Uganda.
"Smile tuna uhakika kuwa kutoa intaneti ya kuaminika na yenye kasi zaidi, itachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya biashara zilizopo Arusha na pia kuwapa wakazi wa Arusha huduma yenye kasi, ya kuaminika na gharama nafuu,” alisema Bi McGloin.
Katika sekta inayokuwa kwa kasi ya mawasiliano hapa Tanzania, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inaongoza kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne  zaidi kuliko 3.75G. Smile inatoa wastani wa kasi ya kupakua ya 6Mbps na kiwango cha 3Mbps kasi ya kupakia. Kwa teknolojia hii, watumiaji wana uhakika wa kasi ya upakuaji na muhimu zaidi, kasi ya upakiaji wa mafaili, barua pepe, taarifa, nyimbo na michezo; matumizi ya nyenzo mbalimbali za kwenye mtandao, na kwa kuangalia video/TV bila kugomagoma.
"Tunajivunia kuwaletea intaneti yenye kasi zaidi jijini Arusha ambayo inalingana na kasi na ubora wa intaneti barani Ulaya. Smile sio tu kwamba tutatoa huduma ya intaneti peke yake, bali tutatoa huduma ya intaneti yenye kasi zaidi, ya kuaminika na kwa bei ya kiushindani na pia tuna nia ya kutoa huduma kwa wateja zenye kuridhisha,” aliongeza Bi. McGloin.
Kama sehemu ya mpango wa kuwajibika kijamii wa kampuni ya Smile, kampuni inatoa huduma za bure za intaneti yenye kasi katika shule za kiserikali: hadi sasa, Smile imewezesha shule 10 jijini Dar es Salaam na inaleta mpango huo katika jiji la Arusha.
Wateja wa Arusha sasa wanaweza kujiunga na Smile kwa kutembelea maduka yetu ya rejareja ambayo yanazidi kuongezeka ,duka la Smile mtaa wa  India, jiji la Arusha , au kwenye kioski ndani ya duka la E-Tronic, gorofa ya kwanza, Njiro Complex, Arusha, au wasiliana na Huduma kwa Wateja kwa barua pepe (customercare@smile.co.tz) au simu +255 (0) 222 199 840.
Kupata taarifa zaidi kuhusu Smile tembelea tovuti: www.smile.co.tz.
Posted by MROKI On Thursday, November 28, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo