WANARIADHA kutoka nchi 21
wanatarajiwa kushiriki mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa
kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi
wa habari jana, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema,
kujitokeza kwa wanariadha kutoka mataifa mbalimbali kumeongeza hamasa kubwa ya
mbio hizo.
Melleck alisema,
wanariadha kutoka mataifa hayo ndio ambao wamejiandikisha mpaka sasa na
wanaamini wengi wataendelea kujitokeza ili kufanikisha lengo lake.
Alitaja nchi wanazotoka
wanariadha waliojiandikisha mpaka sasa ni Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika
Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi na
Marekani.
Wanariadha wengine
wanatoka Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria,
Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.
“Hii ni faraja kubwa
kwetu, kwani inaonyesha kwa kiwango kikubwa lengo letu la kupigania amani,
umoja na mshikamano miongoni mwetu linakubalika na watu wengi duniani,”
alisema.
Aidha Melleck alise,a
usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa
kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na
washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
“Tunachukua nafasi hii pia
kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo
zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani
hakuna chochote kinachoweza kufanyika,” alisema.
0 comments:
Post a Comment