Mkuu wa
Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale
(katikati), Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew
Massawe (kulia) na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye (kushoto)
wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi rasmi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’
ya NBC ikiwa ni moja ya matukio yatakatokwenda sambamba na maadhimisho ya mwezi
wa huduma kwa wateja wa NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Zawadi zote katika promosheni hiyo zitagharimu
zaidi ya shs milioni 300.
Meneja
katika kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na
Wateja Wakubwa cha NBC, Dorothea Mabonye (kushoto) akitoa ufafanuzi jinsi ya
uendeshaji wa promosheni ya Weka Upewe wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es
Salaam leo. Katikati ni Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja
Wakubwa, Andrew Massawe.
0 comments:
Post a Comment