Kampuni ya Mwananchi
Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi
katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu. Kwanza ni gazeti lake mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala
kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo,
wamechukua fursa na kuongelea kuhusu KUREJEA
KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO
na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega
kwa bega.
KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali,
kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama
kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea
kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi
wa uandishi na uhariri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayou yataendelea kusambazwa nchi
nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake
walioenea kote Tanzania.
Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao moja kwa moja.
PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la
MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA MWANANCHI isimame
kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba
promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea.
Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya,
zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa
zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.
PICHANI JUU: Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited(MCL)Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji leo wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky(Kulia kwake) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bernard Mukasa(kushoto)
Mkurugenzi wa Mwananchi, Tido Mhando akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhusiana na kuanza kwa uchapishwaji wa gazeti hilo linalosadikiwa kuuzwa zaidi Tanzania
0 comments:
Post a Comment