Na Mwandishi Wetu
Bendi ya taarabu ya Mashauzi
Classic kesho (Jumatano) itatambulisha nyimbo zao mpya kwenye onyesho maalum ya
kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.
Onyesho hilo ambalo
linajulikana kama ‘Usiku wa Isha Mashauzi’, imeandaliwa na Keen
Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa kinywaji cha Konyagi, Straika,
Kwetu Mbambabay na Saluti5.
Mratibu wa onyesho hilo,
Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho litakuwa la kipekee na maalum kwa
kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj.
Amesema katika onyesho hilo,
Mashauzi atatambulisha albamu yake mpya ijulikanayo kama “Asiyekujua
Hakuthamini” ambayo ina nyimbo kama “Mimi Bonge la Bwana,”
utunzi wake Hashim Said, “Ropokeni Yanayoyahusu” ( Saida Ramadhani)
na “Haya ni Mapenzi Tu” (Zubeda Malik).
Zawadi mbalimabli zitatolewa
kwa mashabiki wa bendi hiyo inayojulikana kama Wakali wa Kujiachia.
“Tumeandaa zawadi
mbalimbali kwa mashabiki wetu. Pia bendi ya Mashauzi Classic watatumia onyesho
hilo kutambulisha nyimbo zao mpya,” Kapinga alisema.
“Mashauzi Classic
watapiga albamu zao zote. Matumaini yetu ni kuwa watu watapata burudani ya
kutosha kuliko siku zingine zote,” alisema Kapinga.
Nyimbo zingine zitakazopigwa
ni “Viwavijeshi” (Issa Ramadhani), “Sitasahau
Yaliyonikuta” (Abdul Malik), “La Mungu Halima Mwamuzi”
(Zubeda Malik) na “Sijamuona Kati Yenu” (Rukia Juma).
Naye mkurugenzi wa bendi
hiyo, Isha Mashauzi, alisema kuwa onyesho la Da West litakuwa la kihistoria na
kutaka watu wajitokeze kwa wingi ili historia isiwapite.“Kwa kweli bendi iko
fiti,” alisema Mashauzi.
0 comments:
Post a Comment