KITAYOSCE FC ya Mjini Moshi
imejikuta ikinyukwa mabao 3-0 na Forest kutoka West Kilimanjaro Wilayni Siha
katika mechi ya Kirafiki iliyochezwa katika Uwanja wa King George Memorial jana
jioni.
Kipigo hicho ni cha tatu
mfululizo katika kujianda aa na Ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro
itakayoanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi ya Oktoba 19 katika viwanja vitatu.
Mabao ya Forest yalifungwa
na Edu Barua katika dakika ya 5 ya
mchezo kufuatia gonga gonga katika lango la KITAYOSCE FC, Said Daudi “Agogo” aliifungia
timu yake bao la Pili katika dakika ya 20.
Hatimaye Dennos Noel “ Chibe”
alipigilia msumari wa tatu kunako dakika ya 65.
Kocha wa KITAYOSCE FC, Hamad
Haule amesema timu yake ilivurunda sana katika dakika 45 za kwanza kutokana na
kuwa na pressure ya mchezo.
Hata hivyo ameongeza kusema
yeye haijalishi timu yake kufungwa anachojali ni kukitengeneza kikosi ambacho
kitaleta ushindi hapo baadaye kama ilivyokuwa awali kutokana na ukweli kwamba
timu nyingi zinajali ushindi kuliko kuwatengeneza watoto kuwa wachezaji ambao
taifa litajivunia kuwa nao.
KITAYOSCE FC inaendelea na
mazoezi asubuhi na jioni katika Uwanja wake wa nyumbani wa King George
Memorial ambapo Jumapili itafungua Ligi
ya Mkoa na Kilototoni ya Moshi Vijijini.
0 comments:
Post a Comment