Meneja Mikopo ya Nyumba wa
benki ya CRDB, Silas Katemi (katikati) akimuelezea Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu mikopo nafuu ya
nyumba inayotolewa na benki hiyo wakati wa Maonesho ya Sekta ya Nyumba
“Tanzania Homes Expo” yaliyoanza jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Julius Ritte akimuonesha jarida lenye maelezo ya kuhusu mikopo ya nyumba. Katikati ni Ofisa Mikopo wa benki hiyo, Aziza Mohamed
Baadhi ya wateja wa CRDB wakipata maelezo katika walipotebelea banda la benki hiyo.
Baadhi ya wateja wa CRDB wakipata maelezo katika walipotebelea banda la benki hiyo.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
******
******
WAZIRI
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, ameitaka
Benki ya CRDB kuongeza kasi ya kuielimisha jamii kutumia fursa
zitokanazo na huduma yake ya Jijenge, ili kusaidia harakati chanya za
Serikali kuboresha maisha ya Watanzania.
Profesa
Mbarawa alitoa wito huo, alipotembelea banda la CRDB katika uzinduzi wa
Maonesho ya Tatu ya Sekta ya Nyumba nchini (Tanzania Homes Expo 2013),
yanayofanyika kwa siku mbili kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
“Maisha
bora kwa kila Mtanzania yanajumuisha pia makazi bora kwa wananchi,
hivyo CRDB inapaswa kuwafikia wafanyakazi na wasio wafanyakazi,
maofisini na majumbani, ili kutoa elimu ya kutosha ya mikopo hii ya
Jijenge,” alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza
kuwa, Watanzania wengi majumbani hawajafikiwa na elimu ya upatikanaji
wa mikopo nafuu ya nyumba na pesa za kujengea, hivyo Huduma ya Jijenge
ina nafasi kubwa ya kuisaidia Serikali katika kuwapatia wananchi makazi
bora na ya kisasa.
Kwa
upande wake, Meneja wa Mikopo ya Nyumba wa CRDB (Mortgage Business
Unit), Silas Katemi, alisema benki yake inaupokea ushauri huo wa
serikali na tayari ilishaanza kuufanyia kazi kwa kuzitembelea zaidi ya
taasisi 40 kutoa elimu hiyo kwa wafanyakazi.
“Jijenge
ni huduma mpya na CRDB imefanya harakati za kutoa na kufikisha elimu
kwa wateja na wasio wateja. Tunaahidi kuendelea kutumia fursa tulizonazo
katika kutoa elimu zaidi na kufikia mwisho wa mwaka huu tutakuwa
tumeitangaza zaidi,” alisema Katemi.
Alifafanua
kwamba, Huduma ya Jijenge inamuwezesha mkopaji kupata pesa ama nyumba
na kulipia hadi kipindi cha miaka 20, ingawa kuna uhuru wa kuamua kwa
mteja kulipa katika kipindi kifupi kutokana na pato lake, huku mkopo
wake ukiwa na bima.
Aidha,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGroup inayoratibu maonesho hayo,
Imani Kajula, alisema kuwa Tanzania Homes Expo ni jukwaa huru,
linalowakutanisha wazalishaji na watoaji wa huduma katika Sekta ya
Makazi na wateja wao.
Alibainisha
kuwa, EAGroup wanajivunia ongezeko kubwa la kampuni shiriki katika
maonesho hayo, kutoka 25 katika mwaka wa kwanza (2011), hadi kufikia
kampuni 70 mwaka huu, linalothibitisha ubora wa maonesho na tija zake
katika uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment