Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt.
Festus Ilako (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha
wakunga kupitia kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania” siku ya
Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili
ya kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy
Mapunda, kulia ni Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline
Woiso (kulia) akisisitiza jamii nzima juu ya kutambua umuhimu wa kuwasomesha
wakunga nchini ambapo azma hiyo itafanikiwa kwa kuunga mkono kampeni ya “Simama
kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF
Tanzania Dkt. Festus Ilako.
Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy
Mapunda (kushoto) akiwashukuru washirika wanaoendelea kuunga mkono kameni ya “Simama
kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”, baadhi ya washirika hao ni ITV/Radio One,
Clouds Media Group, Banki Kuu Tanzania (BOT), Serena hoteli, benki ya NBC,
Toyota Tanzania Tanzania One, DSTV, PPF, TACAIDSWHO na MSD. Kulia ni Mkurugenzi
wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.
Baadhi
ya waandishi wa habari na washiriki wa mkutano unaohusu chakula cha hisani cha
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga uliofanyika leo jijini Dar es
salaam. Kampeni ya kuchangisha fedha inaongozwa na kauli mbiu inayosema “Simama
kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Chakula hicho cha hisani kitafanyika siku
ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha
kwa ajili ya kampeni hiyo.
0 comments:
Post a Comment