Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge
hilo, Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
Katibu wa wabunge wa Afrika Mashari kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
Nasisitiza.....
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakibadilisha mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika
Mashariki kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Adam Kimbisa, Nderakindo Kessy na Makongoro Nyerere.
Mbunge la Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Makongoro Nyerere akipeana mkono na Katibu wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Shy-Rose Bhanji.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake
rasmi ambapo sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika
Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema
hayo katika mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, leo.
Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA,
Tanzania pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.
Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es
Salaama au Zanzibar.
Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike
Arusha, kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha
2013/2014, ndio itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.
Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni
vikao vya bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika
Bunge.
Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu
ni kuwa linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu
na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.
Naye Katibu wa watanzania, Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo
la kujivunia kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya
mazungumzo. Hii ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka
miongoni mwa wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa
mwaka mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la
pili.
Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee
kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.
Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013
vilikuwa vitano kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika
kila baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.
0 comments:
Post a Comment