Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi amewaeleza wakala wa Hifadhi ya Chakula
NFRA kuzingatia ubora na usafi wa ununuzi wa mahindi kwani mahindi
yanayonunuliwa na Serikali ni kwa ajili ya Chakula.
Alisema hayo jana wakati wa Ziara yake ya
ukaguzi wa vituo vya Mahindi vya Mtenga, Namanyere na Kasu vilivyopo Katika
Wilaya ya Nkasi alipokuwa akipokea taarifa ya Ununuzi wa Mahindi katika vituo
hivyo. Waziri Lukuvi alisema “itakuwa sio vizuri kununua mahindi ambayo yako
chini ya kiwango na yaliyo na uchafu mwingi
kwakuwa Serikali inanunua mahindi kwa ajili ya matumizi ya chakula ni
sivinginevyo, hivyo lazima Mahindi haya yawe masafi na yenge viwango bora kwa walaji”.
“Mwaka huu Serikali imetoa bei nzuri ya Ununuzi
wa Mahindi ya shilingi Mia Tano kwa kilo kwa kuzingatia uhitaji, kutokana na bei
hiyo Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA inatakiwa kununua mahindi
yaliyo safi ili kuweza kupanga viwango tofauti ambavyo vitawasaidia katika
uuzaji wa Mahindi hayo kwa watu wengine. Kwa kupanga kupanga hovyo Wakala wa
Hifadhi ya Chakula ya Taifa watapata wanunuzi wazuri, alisema Waziri Lukuvi”.
Alisisitiza kuwa kwa mwaka huu Serikali
ndiyo mnunuzi mkubwa wa Mahindi katika Kanda zote Tanzania na Wakala wa Hifadhi
ya Chakula ya NFRA ndiyo inayoongoza, katika ununuzi huo ambapo ameagiza NFRA
kuanza haraka usafirishaji wa mahindi kwenda Mkoa wa Shinyanga mapema kabla
kipindi cha mvua hakijaanza.
Akipokea taarifa ya ununuzi katika kituo cha
Kasu, Waziri Lukuvi alielezwa kuwa kituo hicho kilipanga kununua Tani za
Mahindi elfu 2000 hadi kufikia Mwezi Septemba,2013 hadi sasa kituo hicho
kimeshanunua Tani 1,904 zenye thamani ya shilingi milioni 952,483,500 na
kitaendelea na ununuzi hadi kufikia malengo ya Ununuzi wa Tani zilipangwa.
Akikamilisha ziara katika Mkoa wa Katavi, Waziri
Lukuvi aliwapongeza wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa jitihada zao za kilimo
walizozionesha na kuwahakikishia kuwa katika kila msimu watalipwa fedha zao kwa
wakati ili waweze kuendelea na kazi, pia ameielekeza NFRA kuhakikisha kuwa kila
vibarua wanapomaliza kufanyakazi walipwe ili kupunguza madeni, NFRA ihakikishe
kuwa kila vibarua wanapomaliza kazi zao walipwe mara moja wasisumbuliwe kwani
fedha wanazopata zinawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment