Maelfu ya wananchi waliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi,
Mkoani Kilimanjaro, wakifuatilia kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa
madini wa Mererani, Erasto msuya , aliyeuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi.
Mtuhumiwa namba moja,
Sharifu ‘Athumani’ Mohammed (31), wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara
Erasto Msuya, akiwasili mahakamani, katika Mahakama ya hakimu mkazi
Moshi, Kilimanjaro.mtuhumiwa huyo na wenzake 6 anatuhumiwa kumuua msuya mnamo 7 kwa kumpiga risasi.
Maelfu ya wananchi waliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi,
Mkoani Kilimanjaro, wakifuatilia kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa
madini wa Mererani, Erasto msuya , aliyeuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi.
KESI ya mauaji
ya mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya (43), imelazimika kusikilizwa katika
mahakama ya ndani baada ya kutokea sintofahamu huku mmoja wa waandishi wa
habari aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo akishambuliwa na ndugu wa Marehemu.
Kesi hiyo
iliyotajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu Mkazi Moshi, Agosti 21
mwaka huu, ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya wazi lakini kutokana na
kuwepo kwa umati mkubwa mahakamani, kesi hiyo ilihamishiwa mahakama ya ndani
jambo lilowakera ndugu wa marehemu.
Baada ya kuambiwa kesi hiyo imehamishiwa
mahakama ya ndani, Ndugu wa Marehemu walionesha kukerwa na kitendo hicho na
kuanza kufanya vurugu na kulazimisha maaskari wa mahakama kuingilia kati
wakisaidiwa na wale wa kutuliza ghasia (FFU).
Katika tukio
hilo, waandishi wa habari wachache walioruhusiwa kuingia kusikiliza kesi hiyo
walijikuta katika wakati mgumu, huku mmoja wao, Venance Maleli wa kituo cha
Redio cha Moshi FM akishambuliwa na wanandugu hao ambao pia walitishia kumnyang’anya
kamera yake.
Tukio hilo
halikuishia hapo kwani, Mwandishi wetu, alifanyiwa fujo na ndugu wa
Marehemu ambao hawakutaka kupigwa picha wakati wakifanya juhudi za kumkimbiza
hospitalini Mama yao, aliyepoteza fahamu baada ya kupata taarifa za kuahirishwa
kwa kesi hiyo.
Aidha baadhi
ya waandishi wa habari waliokuwa mahakamani hapo walilazimika kuondoka kwa
kujificha kwa kuhofia usalama wao.
Katika kesi
hiyo dakika hiyo iliyochukua takribani dakika 25 tu, watuhumiwa wengine wanne
waliunganishwa katika shtaka hilo la mauaji kwa kukusudia kinyume na kanuni
namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai.
Watuhumiwa
hao ni Joseph Damas maarufu Chusa mkazi wa Jijini Arusha, Jalila Zuberi Said
(28), mkazi wa Babati, lakini pia anakaa Manyara na Kondoa , Sadiki Mohammed
Jabir “msudani” au “mnubi”(32), mkazi wa
Dar es salaam na Langata wilayani Hai na Karim kihundwa (33) mkazi wa kijiji
cha Lawate wilayani Siha na kufanya jumla ya watuhumiwa kufikia 7 mpaka sasa.
Hata hivyo maelfu ya wananchi waliofurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, walionesha kukerwa na kitendo cha kutoruhusiwa kusikiliza kesi hiyo ambapo mara tu baada ya kesi hiyo kuahirishwa walionekana kukimbilia mlango wa kutokea.
Hata hivyo maelfu ya wananchi waliofurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, walionesha kukerwa na kitendo cha kutoruhusiwa kusikiliza kesi hiyo ambapo mara tu baada ya kesi hiyo kuahirishwa walionekana kukimbilia mlango wa kutokea.
Watuhumiwa
hao wote 7 waliondolewa mahakamani hapo kwa ulinzi mkali wa Jeshi la polisi
wakiwa wamepakizwa katika Gari ya polisi, namba za usajili T 743 ADC iliyokuwa
na Madirisha Meusi (tinted).
Kesi hiyo inayoendeshwa
na wakili wa Serikali, Stella Majaliwa akisaidiwa na Janeth Sikule katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi, Ruth Mkisi imeahirishwa hadi October 2 mwaka huu kwa ajili ya
kutajwa tena.
0 comments:
Post a Comment