Airtel
Tanzania inatangaza uteuzi wa Bw. Frank Filman kuwa mkurugenzi wa kitengo cha
teknolojia ya IT aliyechukua nafasi hiyo rasmi kuanzia sasa
Filman
ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama munagalizi wa system (system
Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja wa Mradi wa Technolojia ya
IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana
ambapo alisimamia na kutoa mchango mkubwa uzinduzi wa mtandao wa Airtel
nchini Ghana.
Mwishoni
mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa Huduma za
kimtandao (Network service Manager ) za Airtel Tanzania.
Baadaye
alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Techonologia na biashara na
huko aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 100%
kwa mienzi 12 tu.
Katika
miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwiliAirtel Ghana na zaidi
ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.
Akizungumzia
juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema
"Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia ya IT ni
ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania
kuendeleza,
kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi. Sisi tunayo furaha
kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa katika moja ya makampuni
yanayokuwa kwa kasi na nyeti kama hii.
Teknolojia
ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano ya simu kwa sababu
huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha yaani Airtel
Money na internet zinategemea teknolojia hiyo."
Aliendelea
kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika kwamba ataifanya kazi
hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.
"Tunaamini
Bw. Filman atafanya vyema kazi yake kutokana na uzoefu alionao lakini vilevile
Airtel itaendeleza dhamira yake kuwaendeleza na kuwawezesha wafanyakazi wengine
kushika nyazifa kama hizi nchini na kwenye nchi nyingine za Afrika na Asia
ambapo Airtel inafanya biashara. pia Airtel tutaendelea kuwapa mafunzo
wafanyakazi wetu ambayo yatawafanya wawe kwenye viwango vya kimataifa"
Alisema Bw. Golaso.
Akizungumzia
uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata nafasi hii na
nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha kupata wadhifa huu Airtel
Tanzania . kwa miaka mingi nimepitia mafunzo mbalimbali, na nina uzoefu
nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi nyingine Airtel inayofanya biashara.
Hivyo niko tayari na nimejiandaa vyema kukabiliana na changamoto zote katika
utendaji wa kazi hii na kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa
watanzania."
Airtel
tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni ,
kasi ya kazi na kibiashara. Airtel imewekeza katika kukuza uwezo wa
wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi
daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika
kimataifa alisema bw Sunil Colaso mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania
Airtel
imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha wafanyakazi
wa Airtel wanatoa huduma bora za kitaalamu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kumekuwa na fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wafanyakazi wa Airtel Tanzania
katika vitengo vya masoko, Mauzo, IT, pamoja na kuwa na mfumo wa kuwapeleka
baadhi ya wafanyakazi wake nchi tofauti kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa kufanya
kazi kwa mienzi 6 hadi 18 katika Airtel Afrika na India.
Mauzo,
masoko na huduma kwa Wateja kupitia Chuo Kikuu cha Centum .Airtel pia imekuwa
ikiendesha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa Ambapo wafanyakazi wamekuwa
wakipewa ujuzi na maarifa muhimu yanayowasaidia kutoa huduma bora kwa wateja
ambazo zinaleta maendeleo makubwa na kuonesha utofauti katika soko la ushindani
la mawasiliano ya simu.
0 comments:
Post a Comment