Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania Teddy Mapunda akiwagawia soda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana. Wafanyakazi wa kampuni hiyo walisherehekea sikuu hiyo na wanafunzi hao ili kuonyesha upendo.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi hiyo wakati wa sherehe za Eid Mubarak ziliyofanyika shuleni hapo jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam wakiwahudumia chakula cha mchana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliamua kusherehekea sikukuu ya Eid Mubarak na wanafunzi hao jana ili kuonyesha upendo
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa na kampuni ya Montage Tanzania wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakicheza mziki aina ya Kwaito jana wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo.
0 comments:
Post a Comment