UTANGULIZI
Mfuko wa Pensheni wa PPF ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa
mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372 kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena
na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.
majukumu ya mfuko
PPF ina majukumu
yafuatayo:-
kuandikisha wanachama,
kukusanya michango,
kuwekeza michango
inayokusanywa na
kulipa mafao ya pensheni
na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.
WIGO WA UANACHAMA
Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta
zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na
sekta isiyo rasmi
Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba baadhi ya mafao ambayo
Mfuko unatoa ni
Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo
mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia
umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.
Mpaka sasa PPF ina wastaafu wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni
3.7
Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi
tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.
Mafao ya Ugonjwa
Hutolewa pale
ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na
imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena
Mafao ya Elimu:
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa
amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.
Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi
4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014
Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.
Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto
wanachama
UWEKEZAJI
Jukumu linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF
unawekeza kwa mujibu wa sera ya uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA
na BOT. Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza
katika Majengo kama vile ofisi mfano PPF Tower,PPF Plaza Mwanza,vile vile
wekeza kwenye hoteli,nyumba za kupanga vile vile tume tumeshiriki kwenye ujenzi
wa vyuo vikuu kama vile UDOM-kwenye chuo cha Mifumo ya Komputa na chuo kikuu
cha sayansi na Teknologia Nelson Mandela kilichopo Mkoani Arusha.
Tumeshiriki kwenye uwekezaji katika sekta ya
Kilimo Kagera Sugar, 21st Century kiwanda cha Nguo Morogoro Uwekezaji
mwingine ni kwenye Mikopo ya Saccos kwa wanachama wetu ambapo PPF unakopesha
wanachama kwenye maeneo ya Kazi ambapo inasaidia kukuza uchumi
MAFANIKIO
YA MFUKO
Mfuko umetimiza miaka 35 mwaka huu na ulianza kwa
mtaji wa shilingi million 50 mwaka 1992.lakini Mfuko unaendelea vizuri kwa kuwa
na uwezo wa kulipa mafao kwa wakati bila kulazimika kuuza vitega uchumi au
kukopa mahali popote
Kwa upande wa thamani ya Mfuko:
Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa
sasa thamani ya Mfuko ni shilingi trillion
1.3 ukilinganisha na mwaka jana 2012 Desemba ambapo thamani ya Mfuko
ilikuwa trillion 1.09
IDADI
YA WANACHAMA
Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama
ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012
Matumizi
ya mifumo ya habari:
Mfuko umefanikiwa sana katika nyanja ya teknolojia
kwa kuweza kulipa mafao kwa kutumia mtandao, hivyo kulipa kwa wakati.
Vile vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani
‘paper work’ kwa kurahisisha malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma
tunatumia mfumo wa ‘E-banking’ yaani
pesa zinatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.
Kupitia mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama
anaweza kupata taarifa zake za michango, dai au pensheni kwa mstaafu kupitia
simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo ni www.ppftz.org
Mwanachama anaandika neno michango
anaacha nafasi anaweka namba ya uanachama na kutuma kwenye namba 15553.
Si hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata
taarifa za michango ya wafanyakazi wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila
kwenda katika ofisi za PPF hii inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa
uwasilishwaji wa michango ya wanachama.
Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya
habari mwaka huu 2013 katika wiki ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF
ulitunukiwa hati ya utambuzi kama Mfuko
bora kwenye matumizi ya Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais,
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya
habari kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.
Utoaji
wa Mikopo ya SACCOS
PPF ni waanzilishi wa mikopo ya SACCOS tulianza
kutoa mikopo ya saccos mwaka 2004.
Tunatoa mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama
wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mpaka sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye
SACCOS 46
Tuzo
katika Utawala bora
Kwa kutambua uwazi katika uendeshaji wa Mfuko
Umoja Mifuko ya hifadhi ya Jamii Duniani (issa) uliweza kutupatia Tuzo katika
utawala bora kwa kuendesha shughuli mbali mbali kwa uwazi kama vile mikutano ya
wanachama na wadau PPF huu ni mwaka wa 23 tuna desturi ya kukutana na wanachama
na wadau wetu.
Hati
safi kutoka kwa CAG kwa kuwa na mahesabu yaliyo safi
Uwekezaji
ni mzuri ambapo tumewekeza katika sehemu mbalimbali kama vile hoteli za kitalii
mfano East African Hotel Arusha na Gold Crest Mwanza ambapo watalii wengi
wanafika hivyo inasaidia kwenye ukuaji wa Uchumi.
Tumewekeza kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu
kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha
miradi ya nyumba za bei nafuu.
Tulijenga nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza
kwa bei nafuu ya kati ya shilingi
millioni 16 mpaka million 33. Zoezi hili ni endelevu kwa mikoa mingine
Fao
la Elimu:
PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kuwa na Fao la elimu
kwa watoto wa wanachama wetu.Ambapo lilianza kutolewa mwaka 2003 ambapo tangu
tuanze kwasomesha kiasi cha shilingi billion
3.6
LENGO
Katika Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha
miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo ya Mfuko ni kama ifuatavyo:
Thamani ya Mfuko ni kukua kutoka trillion 1.09 Desemba 2012 na kufikia trillion 2 ifikapo Desemba 2015 Na Idadi ya wanachama kuongezeka
kutoka wanachama 203,981 Desemba 2012 kufikia laki 4 Desemba 2015. Lengo
kuongeza mara mbili thamani ya Mfuko
Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanachama na
wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa Mliotupa Hivyo tunaomba tuendelee
kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado hamjajiunga
na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu ya sasa na
baadaye.
0 comments:
Post a Comment