Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki
ya KCB, Christina Manyenye, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya
Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), moja ya vifaa tiba vyenye
thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa
ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya
Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani, akiangalia moja ya vifaa tiba vya
kumwekea mgonjwa gesi, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye (katikati), vifaa vilivyotolewa
na benki hiyo kwa hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa, akimkabidhi moja ya
boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi, Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk.
Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya
Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa
tiba vya kuwekea mgonjwa gesi, vilivyotolewa na benki ya KCB kwa hospitali hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
0 comments:
Post a Comment