Juni 26, 2013 ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Mwana dada Sabrina (Christina) Shogholo Mgonja wakati alipokutana na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki wakati wa tafrija maalujm ya kumuaga kabla ya kuunga na mumewe kipenzi wa maisha yake. tafrija hii ilifanyika Ukumbi wa Magereza Ukonga.
Bi Harusi Sabrina akirembwa katika moja ya salon maridani maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam.
Mdogo wa Bi Harusi, Neema Mgonja (kulia) akiteta jambo na shangazi zake Mariam Kikula (kushoto) na Fadhila Onesmo pamoja na dada yake mkubwa Rose Mgonja nje ya ukumbi.
Hapa ni mtu na dada yake...!! Chief Shogholo Chali akiteta jambo wakati akimuingiza mjukuu wake ukumbini tayari kwa kumpa mkono wa heri kwa kijana aliyempata.
Kuingia kulikuwa kwa staili ...
Sabrina Mgonja akiwa na msimamizi wake, Batuli.
Sabrina akijiandaa kukata keki.
Dada na wadogo zake Sabrina wakifuatilia matukio katika tafrija hiyo.
Ilikuwa ni furaha tu...
Agustino 'Ikechukwu' Shogholo Mgonja, baba wa Bi harusi Sabrina (kushoto) akiwa na mjomba wake Chief wa Mbaga, Chief Eliewaha Shogholo Chali na mkewe wakati wa tafriha hiyo.
Glasi ya pongezi ilipita kwa biharusi
Onesmo Nathan akitoa pongezi na heri kwa Binamu yake Sabrina.
Aliyesema Kwaito Kinyenze haichezi nani? Shangazi wa Bi harusi ambaye ni mama wa Bloger Father Kidevu, akiyarudi kwaito sambana na mdogo wake Mama Nasra na Nasra mwenyewe (kushoto) na Hadija.
DJ naona hapa alizima ghafla...
Shangazi Mkubwam, Mary Nathan akitoa nasaha zake..
Kaka wa Sabrina, Freddy Mgonja akisema neno kwa dada yake.
wapare nao wanangoma zao hapa zilisindikiza nasaha...
Kijana mtanashati Mohamed Jumbe ndiye alisababisha Sabrina kuagwa na familia yak na hivi sasa wawili hawa ni mke na Mume.
Ikechukwu manineno yalimshinda hapa ikabaki ishara tu ya mikono...
madada wakitoa pongezi...
Mutu ya Miraba 5, Rome Mpungu akiyarudi kwanza magoma... kabla ya kumuaga dada yake.
Debora Mroki nae akitoa mkono wa heri kwa Sabrina
Sabrina akipiga picha na wadogo zake Glady (kati) na Neema.
Wakaongezeka na dada zake wengine na kaka mkubwa.
Mashallah.
ReplyDeleteM. Sheki