Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
*******
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa
Marekani kwa huduma bora iliyotoa wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa
nchini.
Akitoa shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora
na za uhakika kutoka TTCL wakati wote wa
ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza kuwa
huduma walizozipata zimethibitishwa na
taarifa kutoka ofisi inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi
walizopita Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya
kiwango cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya
Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Akipokea salam hizo
za shukrani kutoka kwa ujumbe huo wa Marekani, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt.
Kamugisha Kazaura amesema, TTCL ilifanya
kazi yake kwa uhakika na ina uwezo wa kuhimili mahitaji ya watanzania na
Kimataifa pia.
Ameongeza kuwa
TTCL inaendelea na juhudi za kujikita zaidi katika huduma ya data/ intanet na
kuendelea kuboresha gharama ili kila mtanzania apate fursa ya kunufaika na
mawasiliano ya simu pamoja na data.
Katika Shukurani
zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha
Kazaura na kwa baadhi ya wawakilishi
kutoa fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa
TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment