Meneja Uhusiano wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi
aina ya TECNO, akionyesha moja ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu “Smartphones”
ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo imebuniwa
kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu nchini
Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, Patrick Karogila, akionyesha
moja ya simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphone” ambayo imeingizwa katika
soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo pamoja na nyingine zimebuniwa ili
kukidhi mahitaji ya watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Afisa Uhusiano wa
kampuni hiyo Boukali Mounir.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi
aina ya TECNO, akionyesha moja ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu “Smartphones”
ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo imebuniwa
kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni
Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Patrick Karogila.
Mabalozi wa Tecno wakipozi na zawadi
Afisa Uhusiano wa
kampuni hiyo Boukali Mounir, akielezea vitu mbalimbali vilivyopo katika simu hiyo.
**********
Kampuni ya uuzaji wa simu za
mkononi ya TECNO imeendelea kuwekeza zaidi katika soko la Tanzania ili kukidhi
haja ya mawasiliano na ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu ya matunda ya
ushirikiano mzuri kati ya nchi ya Tanzania na China.
Kukua kwa uwekezaji wa kampuni hiyo kwa kasi katika
siku za karibuni kumefuatana na utengenezwaji wa simu za teknolojia ya hali ya
juu “Smartphones” ambapo sasa kampuni hiyo inazitengeneza na kuuzwa katika soko
la nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania kwa bei nafuu.
Pamoja na simu nyingine za teknolojia ya hali ya juu,
simu mpya ambayo imeingizwa katika soko ni aina ya TECNO P3 ambayo
imetengenezwa kukidhi mahitaji ya watumiaji kwa kuwa na teknolojia ya hali ya
juu ya mawasiliano iliyowezeshwa kwa teknolojia ya Android 2.3 na kuiweza
kufanya kazi sawa na simu za teknolojia
ya juu yaani Smartphones.
Kwa kutumia
simu hiyo ya P 3 wateja wataweza kupata uwezo mzuri wa kutumia internet kwa kasi
ya hali ya juu pamoja na kuunganishwa na mitandao mablimbali ya kijamii,
hususani kwa watanzania wa kada ya chini na wale wa vijijini abao matumizi ya
intanet kwao imekuwa changamoto kubwa.
Kampuni hiyo ambayo imeendelea kujiimarisha katika
soko la Tanzania kwa kuanzisha uuzwaji wa simu za teknolojia ya juu inatarajia
kuingia katika ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom katika
kuwawezesha watanzania zaidi kufurahia mawasiliano.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,
Meneja mahusiano wa kampuni ya TECNO, Mounir Boukali amesema, “ Tunatambua kuwa
idadi kubwa ya watanzania wanauhitaji wa kutumia simu zenye teknolojia ya hali
ya juu na yenye uwezo wa kuwa na intanet yenye kasi, matarajio haya hakika
yanaletwa na simu hii ya TECNO P3 ambayo tumeiingiza sokoni punde.
Mounir alifafanua zaidi kuwa kampuni yake pia imeingiza
katika soko aina nyingine ya Smartphones ambazo zinauzwa kwa bei ambayo
watanzania wengi wanaweza kuimudu.
“Soko la mawasiliano na simu limeshuhudia
ongezeko kubwa la matumizi ya intanet katika nyanja mbalimbali, hivyo ni wakati
muafaka kwa makampuni ya simu na watengenezaji wa simu kuungana pamoja katika
kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya wateja wao,”
Akizungumzia
simu hiyo Mounir alisema, TECNO P3 ina kioo cha kushika kwa mkono ( Touch
screen) pia ina Wi – Fi, na imeunganishwa na huduma ya Facebook, Google Play
Store, Gmail , Yahoo , Opera Mini, Whatsup na nyinginezo, na la muhimu zaidi ni
kwamba simu hiyo ina laini mbili za simu.
Pamoja na
kujiimarisha huko katika soko la biashara kampuni hiyo pia imeendelea kujenga
ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu mojawapo ya faida za uwekezaji wa kampuni
hiyo nchini.
Dunia ya sasa imeshuhudia mapinduzi makubwa ya
kiteknolojia ambapo nchi zinazoendelea zinahitaji maendeleo haya katika
kuhakikisha zinaendana na kasi ya maendeleo kulingana na teknolojia hiyo katika
kufikia malengo yao ya kiuchumi na kijamii.
mimi naitwa jumanne magere niko mbeya tukuyu ninapenda kuwa wakala wa tecno je inawezekana nikapewa hiyo nafasi? kazi yangu mimi ni mfanya biashara ya duka simu namba zangu 0752754948/0785413101
ReplyDeletetecno is most lower is the affordable fo every one
ReplyDelete