Nafasi Ya Matangazo

July 30, 2013

Moses Majeshi akimvisha pete ya uchumba mchumba wake Ruth Paranjo katika tafrija ya utoaji mahari iliyoenda sambamba na zoezi hilo muhimu kwa wawili hao huko Kilangare-Hedaru Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro Julai 28, 2013.
 
Bwana harusi mtarajiwa Majeshi ni Mfanyakazi wa idara ya Uhasibu ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro na Bi Harusi mtarajiwa ni Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Morogoro.
 
Production: MD Digital Company: +255 373 999/+255 717 002303 
Whatsapp +255 788 207274.
Pongezi...
 hongera kaka kwa kutuonesha wifi...
 Dada tunashukuru ...
 Baada ya tuklio hilo la kuvishana pete pongezi zilitoka kwa ndugu jamaa na marafiki wa pande zote mbili kwa tukio hilo muhimu.
 Mahari ilitolewa kwa wazazi ambapo kwa mila za Kipare vitu muhimu vyote vilitolewa na Majeshi. Hapa ni Blanketi la mama.
 Majadiliano yalifanyika juu ya ulipaji mahari na hapa ni wazee wakijadili na Majeshi ambapo alimua kunasua hela kidogo ili mahari isikamilike walau libaki deni hata la wekundu kuleta heshima.
 Blanketi ziliendelea kutolewa
 Fedha ya Mahari ilikabidhiwa ambayo ni Ng'ombe kadhaa.
 Ndugu na jamaa kutoka huko Upareni walihudhuria.
 Ndugu na jamaa kutoka Mzumbe Morogoro nao walihudhuria
 Msemaji wa familia ya Majeshi akizungumza
 Wazee wa Kipare wakijadiliana jambo
 Msosi uliliwa kutoa Baraka za tukio la heshima lililofanywa kati ya Moses Majeshi na Ruth Palanjo.
 Ni furaha tu na Msosi ulishuka vyema.
 Majirani wakihudumiwa
 Hatimaye safari ya kurejea ilinza kutoka huko mlimani.
 
 Wageni walipokelewa kwa shangwe za matarumbeta na vinubi.
Hii ndio milima ambayo Moses Majeshi kutoka huko Kagera alikwea na hatimaye kukutana na Msichana mrembo Ruth Palanjo na kuamua kumchagua kuwa mwenza wake.
Posted by MROKI On Tuesday, July 30, 2013 3 comments

3 comments:

  1. Frank Totnan BavonJuly 30, 2013

    Lots of congrats kamanda hiyo ni great achievement!
    Ama kwa hakika Ruth ni wife material naamin mtafurahia sana maisha yenu ya ndoa.
    Much appreciations kwa wazumbe walio msupport mdau ktk safar yake Tuna kila sababu ya kujivunia uwepo wenu!
    All ze best kamanda..

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013

    Hongera Bageshi!

    ReplyDelete
  3. Hongera Moses Majeshi, hapo hapo naomba kuuliza Swali, nami ni Bwana harusi mtarajiwa pale Azani Front 30 Nov 2013. Jamani mahari imenishinda nimeambiwa Milion 1 na laki 4, ila mie nimekomaa laki 7 na Cash nilipanga wapate laki 4 u nusu, Wamekataa Je niachane na Bint. Ushauri wenu muhimu.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo