Nafasi Ya Matangazo

July 23, 2013

 Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja leo amefikwa na umauti baada ya kugongwa na gari aina ya Nissan ambalo linafanya shughuli za kubeba abiria kati ya Gongo la Mboto na Kariakoo jijini Dar es Salaam namba za usajili T 288 AZB na namba ya njia ni S 264D.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wameiambia Father Kidevu Blog kuwa, marehemu aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara ya Nyerere eneo la Mtava karibu na Quality Centre leo asubuhi.
 Askari Polisi wakijadiliana jambo wakati wakifanya taratibu za kuondoa mwili wa marehemu eneo la tukio.
 Daladala hilo T 288AZB ambalo limemgonga mkazi huyo ambaye baadhi ya watu walitambua kuwa anaishi maeneo ya Buguruni Relini.
 Askari akiuliza endapo marehemu huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 45 na 50 anatambulika na yeyote.
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio.
Posted by MROKI On Tuesday, July 23, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo