Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013 wakiwa kjatika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru naMeneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi wakati wa tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephaim Mafuru nae akionesha kipaji chake mbele ya vijana hao.
Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiwa katika picha na wadau wengine wa Guinness na wafanyakazi wa SBL.
Ilikuwa ni furaha tu kwa kila mtu.
Wadau wa Guinness wakibadilishana mawili matatu wakati wa tafrija hiyo.
Regina Gwae kutoka kampuni ya R & R Associate akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge
Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi akilamba picha na mabalozi wa kinywaji hicho.
Baada
ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge yaliyokuwa
yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha
Guinness Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania
katika mashindano hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah
Lounge Jijini Dar es Salaam na waandaji
na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa
kuwapongeza kwa hatua waliyofikia.
Yaliyokuwa
yakifanyika Afrika Kusini hatimaye yalimalizika hivi karibuni huku timu ya
Tanzania ikiishia katika hatua ya nusu fainali kwa nchi kadhaa za Afrika
ikiwemo Ghana, Cameroon, Kenya na Uganda zilizoshiriki mashindano hayo ukiwa ni
msimu wa tatu.
Katika
hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wanahabari iliwashuhudia vijana
walioshiriki mashindano hayo wakiwa na nyuso za furaha na kulakiwa kwa shangwe
na uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Akizungumza
katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Savannah Lounge Meneja Masoko
wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Moses Kebba ameipongeza timu hiyo kwa kufikia
hatua nzuri ya mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu mbalimbali za nchi
zingine za Afrika.
Alisema
kwamba katika hatua hiyo ya nusu fainali waliofikia ni dhahiri vijana hao
wamefanya kazi nzuri huku akivishukuru vyombo vya habari kwa kuwatangaza vyema
wakati wa ushiriki wao kati mashindano hayo ya Guinnes Football Challenge.
Amesema
kwamba katika mashindano hayo nchi kadhaa zilishiriki kama vile Ghana, Cameroun, Kenya & Uganda, ambapo
amekiri kwamba katika mashindano hayo kumekuwapo na ushindani mkubwa licha ya
Tanzania kutoibuka na ushindi ilifanikiwa kufikia katika hatua ya nusu fainali.
Kwa upende wake Meneja wa bia ya Guinnes Davis kambi amesema kwamba wataendelea kusaidia zaidi kuibua vipaji vya soka kupitia ushiriki huo ambao utaleta tija katika soka la Tanzania kwa kutangazika hatimaye kufanya vyema katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa Afrika na sasa wataendelea kutafuta zaidi vipaji vitakavyoshiriki katika msimu ujao.
“Kila mmoja katika kampuni yetu
ya SBL na watanzania wanayofuraha na nakuwapongeza Daniel Msekwa na Mwalimu Akida, kwa kufanya vizuri licha ya kushindwa kufika
hatua ya fainali lakini kazi mlioifanya imeonekana na mmeweza kuiwakilisha vyem
Tanzania katika mashindano ya Guinness Football Challenge”, Alisema Kambi
Katika
fainali ya mashinado hayo yaliyoshirikisha pia timu za Uganda na Kenya timu ya
Tanzania ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE
iliwakilishwa na Daniel Msekwa, Mwalimu Akida, Mohamed Kobembe, Gullam Sosha,
Hamza Rashid,Lukwesa Kanakamfumu, Abubakari Mohamed, Kherry Sadallah, Simon
Chimbo na Emmanuel Temu.
Akizungumzia
mashindano hayo Daniel Msekwa amesema: “Tumepata uzoefu mkubwa katika
mashindano lakini kubwa ni kuhakikisha tunafanya mambo kulingana na mawasiliano
ya kupata vipaji zaidi ambapo timu za Kenya na Uganda zilifanikiwa kufikia
malengo mazuri lakini hayo yote ni changamoto kwetu.”
“Tunaishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa
sababu walifanya kila jitihada kipindi tupo Afrika Kusini kwenye mashindano na
kuona utofauti wa nchi zingine kama Ghana na Cameroon,
0 comments:
Post a Comment