VIMWANA
16 wa kanda ya Temeke, wameanza kujinoa leo(Juni 17) kwenye klabu ya TCC
Chang'ombe, tayari kwa kinyanga'nyiro kitakochafanyika Julai 5, mwaka huu
katika ukumbi huo.
Idadi
hiyo ya warembo ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania
taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester ambaye atakuwa
mmoja wa wakufunzi katika kambi hiyo, ambayo pia inasimamiwa na Suzy Mwenda na
Shadya Mohamed.
Mbali
ya hao, pia kutakuwa na jopo na wakufunzi wa dansi, litakaloongozwa na Bokilo
na Charles yote katika kuhakikisha shoo ya mwaka huu, itaendana na ubora wa
warembo wanaoshiriki shindano hilo, ambapo kwa hakika Redds Miss Tanzania mwaka
huu, bila shaka atatokea katika kanda hiyo, yenye historia ya mafanikio.
Temeke,
imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika
mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini
katika njanja mbalimbali.
Miongoni
mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za
mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look,
baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika
China.
Pia,
Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania
na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani,
Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania,
Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate
alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss
Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya
ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss
Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke
baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi
nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na
Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa
nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004,
Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss
Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
Shindano
hilo, linalotarajiwa kuwa na burudani ya kipekee limedhaminiwa na kinywaji cha
Redd's, Dodoma Wine, Jambo Leo, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito
Entertainment, Kitwe General Traders na CXC Africa tours & Safaris.
Warembo
wa Redds Miss Temeke 2013
1-Axsaritha Vedastus, 2-Belinda Paul, 3-Darling
Mmari,4-Esther Muswa,5-Hyness Oscar,6-Irene Rajab,7-Jamila Thomas,8-Latifa
Mohamed,9-Margreth Gerald,19-Margreth Olotu,11-Mey Karume,12-Mutesi George,13-Naima
Ramadhan, 14-Narietha Boniface, 15-Stella Mngazija,16-Svtlona Nyameyo.
0 comments:
Post a Comment