Warembo 12 wanaotarajiwa kupanda jukwaani Juni 15
mwaka huu kuchuana katika shindano la kumsaka malkia wa urembo mkoani
Kilimanjaro, Redds Miss Kilimanjaro 2013 wameingia kambini leo.
Walimbwende hao wanaotarajia kupambana kumpata Mrithi
wa Redds Miss Kilimanjaro 2012, Anande Michael anayeshikilia taji hilo kwa sasa,
wameweka kambi katika hoteli ya Hugo, iliyoko nje kidogo ya mji wa Moshi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa
Mashindano hayo, Mkurugenzi wa Kampuni wa Rick Plan Company Ltd, Jackline Chuwa
alisema ameamua kuwaingiza warembo kambini mapema ili kuhakikisha kuwa
mashindano ya mwaka huu yanakuwa toofauti na ya mwaka jana.
“Warembo wanaingia kambini Le, ili kuhakikisha kuwa mashindano yanakuwa ya
kipekee, tuimeboresha mamnbo mengio na lengo ni kumpata Redds Miss Tanzania
2013, warembo wapo pale Hugo Hotel,” alisema Chuwa.
Mkurugenzi huyo alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika
Juni 15 mwaka huu, kuanzia saa moja kamili jioni katikia ukumbi wa La Liga
Carnivore na kuongeza kuwa viingilio ni sh. 15,000 kwa viti vya kawaida n ash. 30,000
kwa viti vya watu maalum (VIP).
Kuhusu Burudani, Mkurugenzi huyo aliwataja wasanii
wa Bongo Movie wakiongozwa na JB, msanii wa kimataifa kutoka Burundi, Kidumu na
Bendi yake, Ngoma za asili na Sarakasi huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri
wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Redds Miss Kilimanjaro 2013 inadhaminiwa na Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original, Panone and Company
Ltd, Bonite Bottlers kupitia kinywaji baridi cha Cocacola na maji ya
Kilimanjaro, Mr. Price, Hugo Hotel na Kilimanjaro Express Bus.
0 comments:
Post a Comment