Meneja
wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya
simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Mwl.Michael
Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika
ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake
ni Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney,
kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto).
Meneja
wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari
wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde katika mkutano uliofanyikajana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.
Wakihakiki
namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde
iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza
kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, Afisa
mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka Bodi ya
Michezo ya Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto).
*************
Mshindi
asherekea kitita cha 1,000,000 huku akiwapongeza kampuni ya bia ya Serengeti
kwa promosheni hiyo.
25 Juni 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili
wa kampeni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja
baada ya kuchezesha droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za
kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika
bodi ya uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.
Baada ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa
sekondari kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi
kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na
Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia kufungua duka kwani
ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo
na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka
sasa nimeshajishindia bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.
Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha Serengeti Mr. Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya
kipekee na mpaka sasa watu 110,000 wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu
ambazo ni shilingi 10,000 na100, 000/= na droo ya kwanza ilichezeshwa mwezi
uliopita huku mshindi kutoka Moshi akiondoka na kitita cha milioni moja, pia promosheni
hii inampa fursa mshindi kununua kile anachokitaka baada ya kujishindia fedha
taslimu kwani tunaamini baadhi ya wateja wetu wana ndoto nyingi sana za
mafanikio ila tatizo huwa ni pesa ili kitimiza ndoto zao.
Lengo
la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini
mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza
bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii
kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa
wateja wake.
Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na
kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa
kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na
unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
0 comments:
Post a Comment