Katibu wa asasi isiyo ya
kiserikali ya Mategemeo Women Association,Viola Lindikikok akitoa mada katika
mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo na kuwashirikisha zaidi ya
vijana 100 kutoka katika kata za lemara na Daraja mbili za jijini Arusha,pembeni
yake ni wahamasishaji katika mdahalo huo
Mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola akitoa semina
ya elimu ya uraia iliyoandaliwa na taasisi ya Mategemeo Women Association ya
jijini Arusha.
****************
Imeelezwa ya
kwamba vijana wengi nchini hawana uelewa wa elimu ya uraia hali ambayo
imepelekea baadhi yao kushindwa kutambua majukumu yao ya msingi na fursa
mbalimbali za kuwaingiza kipato.
Hayo
yalisemwa hivi karibuni na katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo
Women Association,Viola Likindikok wakati alipokuwa akizungumza katika mdahalo
wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo .
Mdahalo huo
uliwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka kata za Lemara na Daraja mbili
ambapo miongoni mwao ni wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo ndani ya kata
hizo.
Katibu huyo
alisema kwamba katika utafiti wao wamebaini ya kwamba vijana wengi nchini
hawana elimu ya kutosha kuhusu suala la uraia hali ambayo imekuwa ikichangia
kushindwa kujitambua.
Hatahivyo,alisisitiza
ya kuwa katika midahalo mbalimbali waliyoifanya vijana wengi wamekuwa wakihoji
kuhusu suala la ajira ambalo alikiri ni changamoto kuu kwa serikali na kila
mdau wa maendeleo hapa nchini.
Naye,mkuu wa
kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola alisema ni vyema vijana nchini
wakapewa elimu ya uraia ili waweze kujitambua na kuepuka kutumiwa katika
harakati mbalimbali za kichochezi.
Baadhi ya
watoa mada katika mkutano huo,Happy Mwajunga na Salmin Sulle walisema kuwa
waliwataka vijana kuacha kulalamika na kukata tamaa katika maisha huku
wakiwasisitiza kuwa wadadisi ili waweze kutambua fursa mbalimbali za
kuwaingizia kipato.
0 comments:
Post a Comment