JUMLA
ya madaktari sita na wataalamu
wawili ,mmoja wa teknolojia na mwingine
wa utawala kutoka Misri wamewasili
nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa tundu ndogo kwenye Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili(MNH) jijini Dare es
Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Hussein Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa madaktari
hao .
“Madaktari hawa watasaidia kutoa tiba na kuwafundisha madaktari wetu
utaalamu huu, hivyo ujio wao utasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kwenda
nje ya nchi,” alisema Dk. Mwinyi.
Aliongeza kuwa madakatari hao watakuwepo katika hospitali hiyo kuanzia Juni 10 hadi 15, mwaka
huu kwa ajili ya kutoa huduma hizo.
Dk. Mwinyi aliushukuru ujio huo kwa kuwa utasaidia
kubadilishana uzoefu na teknolojia na kuboresha
afya ya Watanzania.
Kwa upande wake, Balozi wa Misri
nchini Tanzania, Hossam Omar
alisema ujio wa madaktari hao ni
kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta hiyo, ambapo
watauendeleza katika maeneo mengine ya sekta hiyo na nyingine.
0 comments:
Post a Comment