Nafasi Ya Matangazo

June 10, 2013

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya ngoma za asili kwa wakazi wa kanda ya ziwa. Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa nane sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bwana Fimbo Butallah alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa katika kusherehekea msimu huu wa mavuno. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”.


Bwana Fimbo alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya Ngoma yatahusisha mikoa mitano ya kanda ya ziwa. Yataanza rasmi kutimua vumbi Jumamosi hii tarehe 15 June katika mkoa wa Tabora kisha kuelekea mikoa ya Shinyanga, Kagera, Mwanza na kumalizikia mkoani Mara katika mji wa Musoma. Washindi watakaopatikana katika mikoa watashindanishwa kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa kufanyika jijini Mwanza katikati ya mwezi wa saba. Tarehe rasmi za mashindano haya ni kama inavyoonekana hapa chini;

1.    Mkoa wa Tabora; Jumamosi tarehe 15 June                 Uwanja wa Ipuli Mnadani.
2.    Mkoa wa Shinyanga; Jumamosi tarehe 22 June           Viwanja vya wa Shycom.
3.    Mkoa wa Kagera; Jumamosi tarehe 29 June                 Viwanja vya Kaitaba.
4.    Mkoa wa Mwanza; Jumamosi tarehe 06 July                Uwanja wa CCM Kirumba.
5.    Mkoa wa Musoma; Jumamosi tarehe 13 July               Bwalo la Magereza.
6.    Mashindano ya Kanda; Jumamosi tarehe 20 July        Uwanja wa CCM Kirumba.
Bwana Fimbo alizungumzia pia zawadi za mwaka huu katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda kwamba Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi milioni saba kama zawadi. Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;

ZAWADI
NGAZI YA MKOA
NGAZI YA KANDA
Mshindi wa Kwanza
600,000
1,100,000
Mshindi wa Pili
500,000
850,000
Mshindi wa Tatu
400,000
600,000
Mshindi wa Nne
300,000
500,000
Mshindi wa Tano hadi wa Kumi kila kikundi
150,000
250,000


Bwana Fimbo alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi kufurahi kwa pamoja waburudike na ngoma zetu za asili kutoka sehemu tofauti tofauti. Aliwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
Posted by MROKI On Monday, June 10, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo