Nafasi Ya Matangazo

February 25, 2025











Na. Mwandishi wetu, Dodoma
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amewataka watumishi wa Tume kufanya kazi kwa kujituma na weledi hasa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.
 
Mhandisi Lwamo ametoa rai hiyo mapema leo Februari 25,2025 jijini Dodoma akifungua mafunzo ya matumizi ya mashine maalum za kupima madini ya metali  kwa njia ya Mionzi /X-RAY kwa watalam wa Tume ya Madini wakiwemo  Wahandisi Migodi, Wahasibu, Watakwimu, Maafisa Utawala na Wataalam wa Maabara ‘Lab Technologist.
 
Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa  Tume ya Madini rekodi ya makusanyo ya maduhuli ya Serikali imeendelea kukua hali iliyopelekea wadau wengi wa madini na wananchi kwa ujumla kuwa na taswira  chanya ya Tume.
 
“Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 tulimaliza kwa kukusanya Shilingi Bilioni 753, mwaka huu tunatakiwa kukusanya Shilingi Trilioni Moja, sote tunapaswa kuwa na weledi ili tuweze kufikia lengo, hatuwezi kufika bila uadilifu, kujituma na kutunza vitendea kazi,”amesema Mhandisi Lwamo.
 
Katika hatua nyingine,  Mhandisi Lwamo amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini itaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Masoko ya Madini, Vituo vya Ununuzi wa Madini na Maabara ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini.
 
Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wanajengewa uwezo wa matumizi sahihi ya mashine za kupima madini ya metali ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia sana kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.
Posted by MROKI On Tuesday, February 25, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo