Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundega akiongea na warembo
wanaowania taji la Redd's Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea
kambini kwao ili kuona Maendeleo yao. Lundenga aliwaasa washiriki hao
kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika
fainali yao.
Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache
wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redd's Miss
Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es Salaam. Wengine pichani kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu
Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega,
mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano
hayo Dennis Ssebo.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa wamejipanga mara baada ya kumaliza mazoezi.
***** ******
Na Mwandishi Wetu
REDD’S Miss Tanzania, Brigette
Alfred kesho anatarajiwa kuvua taji jingine, pale kutakapokuwa na kinyang’anyiro
kikali cha kumsaka Redd’s Miss Kinondoni.
Shindano hilo linalotarajiwa
kufanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam linasubiriwa kwa hamu
kubwa ili kujua nani atarithi mikoba ya Brigette.
Mrembo huyo alianza kuvua
rasmi mataji yake wakati wa shindano la Redd’s Miss Sinza na sasa ni wakati
mwingine wa kukabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni ambalo analishikilia.
Akizungumzia shindano hilo,
Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Dennis Ssebo alisema kila kitu kimekamilika
na warembo wote wako tayari kwa ushindani mkubwa ulio mbele yao.
Jana wajumbe wa Kamati ya
Redd’s Miss Tanzania walitembelea kambi ya warembo hao iliyopo katika hoteli ya
JB Bellmont ili kuwatia moyo.
Alipoulizwa kuhusu shindano
hilo, Brigette alisema ana uhakika mkubwa Redd’s Miss Tanzania mwaka huu
atatoka Kinondoni pia.
Washindi wane kutoka Redd’s
Miss Kinondoni watapata fursa ya kuingia moja kwa moja katika shindano la
Redd’s Miss Tanzania litakalofanyika baadaye mwaka huu.
Wakati Kinondoni wakisaka
mrembo wao, kazi nyingine kubwa itakuwa kesho katika kumpata Redd’s Miss Tanga
shindano ambalo litafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, mjini humo.
Mratibu wa shindano hilo, Asha
Said alisema kutakuwa na burudani kubwa itakayotolewa na wasanii mbalimbali
wakiwemo Tunda Man, Nabisha kutoka THT na Fady Dady. Kiingilio katika shindano
hilo kitakuwa Sh 15,000 kwa viti maalumu na Sh 5,000 kwa vile vya kawaida.
0 comments:
Post a Comment