Afisa
Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni,Bi. Merry Komba
akishirikiana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo
Butallah kupanda mti kwenye eneo la Shule ya Msingi Mlimani ilipo ndani
ya eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa
Kampeni ya Exel With Grand Malt inayoendeshwa na kinywaji cha Grand
Malt.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akimwagia maji
mti waliopanda kwa kushirikiana na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kinondoni,Bi. Merry Komba.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani,Hanifa Mponji akiongea na waandishi wa
habari wakati akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia kinywaji chake cha Grand Malt kwa kuweza kupanda miti katika
Shule yake.
Afisa
Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni,Bi. Merry Komba
akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kupanda miti katika Shule ya
Msingi Mlimani ilipo ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni ya Exel With Grand Malt
inayoendeshwa na kinywaji cha Grand Malt.Bi. Komba aliwaasa walimu na
wanafunzi wa shule hiyo kuanzisha klabu ya kutunza Mazingira kwani faida
yake wataiona baadae.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani wakishiriki zoezi la upandaji miti.
0 comments:
Post a Comment