Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi yaliyofanyika Kondoa, mkoani Dodoma, Desemba 30, 2024 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha Maombolezo alipomwakisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko yamefanyika Kondoa, mkoani Dodoma, Desemba 30, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa pole Mwajuma Mafita ambaye ni Mama wa marehemu Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko, aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo, Kondoa Mkoani Dodoma. Desemba 30, 2024
🔴Asema alikuwa alikuwa ni moja ya majaji wa mahakama ya rufani wenye uwezo mkubwa_
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha Maombolezo alipomwakisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko yamefanyika Kondoa, mkoani Dodoma, Desemba 30, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa pole Mwajuma Mafita ambaye ni Mama wa marehemu Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko, aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo, Kondoa Mkoani Dodoma. Desemba 30, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Kondoa Mkoani Dodoma. Desemba 30, 2024
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Desemba 30, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Akitoa Salama pole kwa waombolezaji nyumbani kwa marehemu Kondoa, Mkoani Dodoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameguswa na kifo cha Mheshimiwa Mwanaisha kwani alikuwa ni moja ya majaji wa mahakama ya rufani wenye uwezo mkubwa katika nafasi zote alizozitumikia.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Marehemu Mheshimiwa Mwanaisha alikuwa kiongozi aliyetekeleza wajibu wake kwa weledi na uadilifu “Msiba huu kwetu ni mzito, jukumu letu Wanakondoa, Watanzania, Majaji na wajumbe wa Tume ni kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa kila mmoja kuenzi yote mazuri aliyoyafanya Mheshimiwa Mwanaisha katika kipindi chake chote cha utumishi wa umma kwani kufanya hivyo kutakuwa ni njia nzuri ya kuweka kumbukumbu ya kazi zake.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amesema kuwa Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko aliishi kiapo cha Uhakimu kwa kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo kutatua migogoro kwa uadilifu bila upendeo wowote,
“Mheshimiwa Mwanaisha alikuwa na ubinadamu na utu, maisha yake yalikuwa ni yakusaidia watu wengine, sisi tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani uhai wake umetusaidia sana katika shughuli mbalimbali za kimahakama”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufani) Jacobs Mwambegele amesema kuwa Mheshimiwa Mwanaisha ameondoka katika kipindi ambacho Tume ilikuwa inamuhitaji hasa katika kipindi hiki ambacho Tume hiyo ipo katika mchakato wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
“Tumempoteza Mheshimwa Mwanaisha tukiwa kwenye mzunguko wa nane wa zoezi la kuboresha daftari na tukiwa tunaingia kwenye mzunguko wa tisa utakaohusiaha mikoa minne Rukwa, Songwe, Njombe na Ruvuma, pia mara zote alitoa ushauri wenye weledi wa hali ya juu katika kuhakikisha tume inatekekeza majukumu yake kwa kuzingatia katiba sheria kanuni na taratibu”.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Mheshimiwa Mwanaisha alikuwa ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa masuala ya wanawake, “alibobea katika eneo ambalo alikuwa anafanyia kazi, sisi wanadodoma tutamkumbuka kwa machango wake mkubwa kwenye masuala ya maendeleo”
Marehemu Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Mwanaisha Kwariko alifariki Desemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment