Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania wote kuhakikisha wanatumia nishati safi ya kupikia kama njia mahususi ya kutunza na kulinda mazingira pia kuokoa uharibifu wa misitu.
Katika tamasha maalumu la azimio la Kizimkazi lililofanyika mkoani Lindi wilaya ya Ruangwa leo tarehe 31 Disemba, 2024 Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha kuwa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kimataifa inayofanyika kwa lengo la kuimarisha afnya za wananchi na kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati endelevu.
0 comments:
Post a Comment