Na Immaculate Makilika- Dodoma
SERIKALI yawashukuru
wafugaji wote nchini kwa mchango
wao mkubwa unaoliwezesha Taifa kutoagiza nyama toka nje ya nchi
na badala yake kuliingizia kipato
kutokana na mauzo ya mifugo hai na nyama nchi za nje.
Hayo yamesemwa
Bungeni leo na Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ,
Benedict Ole Nangaro ,wakati wa kipindi
cha maswali na majibu, hata hivyo Naibu
Waziri huyo alisema kwamba mwaka 2011/2012, ng’ombe 3,362 na
mbuzi/kondoo 4,060 wenye thamani ya Sh. Bilioni 3.81 waliuzwa nje.
Aidha tani 31.6 za nyama ya ng’ombe ,tani 647 za nyama
ya mbuzi na tani 151.8 za nyama ya kondoo ziliuzwa nje na kulingizia
Taifa takribani Sh. bilioni 19.3
Fedha iliyookolewa kwa kutoagiza nyama kutoka nje haiwekwi
kama akiba mahsusi bali hutumika kwa
maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo
sekta ya mifugo.
Nchi yetu inajitosheleza kwa mahitaji ya nyama ambayo kwa mwaka tunazalisha wastani wa tani
462,686, kwa mchanganuo wa nyama ya ng’ombe tani 248,108, nyama ya mbuzi/kondoo
tani 92,351, nyama ya nguruwe tani 39,676 na nyama ya kuku tani 82,551.
Hata hivyo, kutokana na mahitaji ya soko hususani wageni
toka nje ,baadhi ya hoteli za kitalii na migodi
huagiza tani 800 za nyama maalumu kwa mwaka ,kiasi kinachogharimu Sh.
bilioni 10.2.
Serikali inaendelea kuwahimiza wafugaji kufuga kibiashara
na kuzalisha nyama bora ili
kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje
ikiwemo migodi.
0 comments:
Post a Comment