Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman
Nyambui (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza
kufunguliwa rasmi milango kwa
makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio
za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika
kila mwezi Desemba zikiambatana na
maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd
ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck.
Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd
ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza
kufunguliwa rasmi milango kwa
makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio
za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika
kila mwezi Desemba zikiambatana na
maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman
Nyambui.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio hilo.
****** ******
Kampuni ya
Intellectuals Limited, ambao ndio waasisi na waratibu wa mbio za Uhuru
zijulikanazo kama “Uhuru Marathon” leo wametangaza kufungua rasmi milango kwa
makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio hizi za
aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na
maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.
Akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi mkuu wa Intellectuals Ltd
Bw. Innocent Melleck, alisema; Nadhani wote mnakumbuka uzinduzi wa mbio hizi za
Uhuru, uliofanyika mwezi Desemba mwaka Jana, ukiwa unaashiria kuanza kwa
mchakato wa maandalizi ya mbio zenyewe ambazo zitaanza kufanyika mwezi desemba
mwaka huu 2013.
Mbio hizi za Uhuru, kama lilivyo jina lake ni mbio
zilizoanzishwa ili kuongeza chachu za watanzania kuwa na moyo wa kulinda Amani,
Umoja na Mshikamano wetu, wakati tunaposherehekea sikikuu za Uhuru wa Taifa
letu. Tangu tulipofanya uzinduzi mwezi desemba mwaka jana, sisi waratibu na viongozi wa chama cha riadha Tanzania
(RT), tulianza mchakato wa maandalizi ya awali ya kufanikisha mbio hizi,
ikihusisha kupanga mzunguko utakaotumika kwa mbio hizo n.k.
Kwa sasa
maandalizi ya awali yanaendelea vizuri, nasi tumeona kuwa huu ni muda muafaka
kufungua milango ya Udhamini kwa makampuni, mashirika na Taasisi mbalimbali
ambazo zitahitaji kushirikiana nasi katika kufanikisha mbio hizi wajitokeze na
kupata taratibu za udhamini. Tuna imani kubwa kuwa wapo wadau wengi wenye lengo
la kufanikisha ajenda hii muhimu ya kuenzi Amani, Umoja na mshikamano wa Taifa
letu. Mbio hizi zina vipengele vikuu vitatu;
i.
Mbio Ndefu (Full Marathon 42
km)
ii.
Mbio za Kati (Half Marathon 21
km) na
iii.
Mbio za kujifurahisha (Fun run
5km)
Mdhamini
atakayedhamini mbio ndefu (full marathon), ndie atakaebeba jina la Mashindano
haya. Hivyo nawasihi wale wote wenye nia ya kudhamini kuanza kujitokeza sasa na
kuchagua mbio zipi wanataka kudhamini ili taratibu nyingine zifuatie. Alisema
Innocent.
Akizungumzia
kuhusu upande wa ufundi, Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa Bw. Suleyman
Nyambui alisema; kwa upande wetu sisi RT, maandalizi ya awali yameshaanza
kufanyika ikiwemo kupendekeza mzunguko wa mbio hizo na kuangalia mambo yote ya
kiufundi yanayohusiana na mbio hizi.
Tunawaomba wadhamini wajitokeze ili kwa
pamoja tuweze kufanikisha mbio hizi zenye malengo mazuri kwa Taifa letu kwa
ujumla. Mbio hizi tutazisimamia na kuziendesha katika hadhi ya kimataifa ili
kuhakikisha kuwa zaidi ya kulinda Amani na Umoja wetu, pia tunalitangaza Taifa
letu kote ulimwenguni.
Kwa kuwa mimi ninaangalia zaidi upande wa ufundi,
nichukue nafasi hii pia kuwasihi wanariadha wa hapa nchini kuanza maandalizi ya
mbio hizi, maana mwezi desemba si mbali, japo najua kuwa wapo ambao walishaanza
maandalizi tangu tulipozindua rasmi mwaka jana. Itakuwa si vyema nafasi za juu
zikichukuliwa na wageni, wakati sisi tunao wana riadha wazuri hapa nyumbani.
0 comments:
Post a Comment