Sehemu la Daraja la Rau, lililoko katika manispaa ya
Moshi, Mkoani Kiliamnajro lililokataliwa na Viopngozi wa CCM wilaya ya Moshi katika
ziara ya kukagua miradi ya manispaa Moshi ili kujiridhisha kama miradi
inayoendeshwa na Manispaa hiyo ianendena na kiwango kinachotakiwa.
Wajumbe wakijadiliana jambo wakati wakikagua miradi mbalimbali ya maeneleo.
Katibu wa CCM, Aluu Segamaba akiongoza viongozi
wenzake kukagua daraja la Rau linadaiwa kujengwa kwa kutumia kiasi cha sh.
milioni 102, lililokatika kabla ya ujenzi wake kukamilika, viongozi wamelikataa
daraja hilo.
****** *******
Na Mwandishi Wetu Moshi
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi,
imelikataa daraja la manispaa iliyojengwa katika kata ya Rau mbokomu
lililojengwa kwa kutumia fedha za serikali kutokana na kutoridhishwa na kiwango
cha ujenzi wake.
Wakizungumza baada ya kukagua daraja hilo, ambalo
pamoja na ujenzi wake kutokamilika na kukabidhiwa kwa wananchi, Viongozi wa CCM
wilayani hapa ambao walikuwa katika ziara maalum ya kukagua miradi ya serakili
iliyojengwa katika manispaa hiyo, walisema inasikitisha kuona kazi muhimu kama
ujenzi wa daraja likitekelezwa kizembe.
Viongozi hao kutoka katika Kamati ya Siadsa ya
Halmashauri kuu CCM wilaya ya na Sekreteriet ya Halmashauri kuu ya CCM
wakiongozwa na Mjumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey Marealle, Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Moshi, Elizabeth Minden a Katibu wa CCM wilaya, Aluu Segamba
wamelikataa daraja hilo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.
Wakiwa wameongozana na Mkadiriaji wa Gharama za
ujenzi wa Manispaa , Mhandisi Charles Huka na Msaidizi wa Mchumi wa Manispaa,
Evera Lyimo. Viongozi hao walisema hata kiasi cha fedha cha sh. Milioni 102,
kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo lililoanza kubomoka hata kabla
ya ujenzi wake kukamilika ni kidogo mno ikilinganishwa na ukubwa wa kazi.
Akizungumza na MTANZANIA kuhusu tamko lao, katibu
wa CCM wilaya ya Moshi, Aluu Segamba alisema kimsingi wao kama chama tawala,
hawajaridhika na kiwango cha ujenzi wa daraja hilo huku akiwataka wananchi
kutopitisha magari yao katika daraja hilo kwa usalama wao na kuongeza kuwa
ujenzi huo unatakiwa urudiwe upya.
Alisema kuwa kilichofanyika katika daraja hilo
ni uhuni mtupu na kuongeza kuwa hawatakubali kuona fehda za umma zikiteketea
ovyo kutokana na uzembe wa watu wachache.
“Kimsingi hili daraja hatujaridhika na kiwango
cha ujenzi wake, huu ni uhuni na kamwe kama chama tawala hatuwezi kukaa kimya
huku fedha za umma zikitafunwa kizembe, utajengaje daraja kwa kutumia milioni
102? Tunawaomba wananchi wasipitishe magari hapa hadi litengezwe katika kiwango
kinachoridhisha,”alisema Segamba.
Naye Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey
Marealle alisema kuwa baada ya kufanya ziara hiyo wanatarajia watakaa na
kujadili kwa kina na kasha kutuma mtaalamu wao katika miradi yote waliyokagua
na kasha watatuma mapendekezo yote kwa wizara ya ujenzi.
Hata hivyo Mkadiriaji wa gharama wa ujenzi wa
manispaa, Charles Huka, ambaye katika ziara hiyo alimwakilisha
Mhandisi wa Manispaa, Alipoulizwa kuhusu ujenzi wa daraja hilo, alisema kuwa
muda wa mkataba wa mkandarasi haujakamilika na kimsingi wao wanaridhishwa na ujenzi
huo.
Huka alisema kuwa kilichotokea ni sehemu ya
udongo kumeguka huku akiongeza kuwa wanachokisubiri ni muda wa mkataba wa
mkandarasi huyo kukamilika ndipo watakapotoa maelezo wa nini kimefanyika ila
kwa sasa wanaridhika na kiwango cha ujenzi na wana imani na mkandarasi wao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo hilo
pamoja na kupongeza manispaa kwa kuwahjengea daraja katika eneo hilo,
wameonesha wazi wasiwasi juu usalama wao na kuliomba serikali kuhakikisha
daraja hilo halileti madhara kwao.
Wakizungumza na gazeti hili, Mchungaji Frank
Machange, ambaye ni mratibu wa mazingira katikiamkaisa KKKT jimbo la Moshi na
mwananchi Emmanuel Erick walisema kitendo cha kujengewa daraja katika eneo hilo
ni la kupongeza lakini kuna hali ya hatari kutokana na daraja kuanza kumeguka.
Miradi mingine iliyokaguliwa na Viongozi wa CCM
katika ziara hiyo ni, Ujenzi wa Nyumba za walimu katika shule ya msingi
Msandaka, shule ya sekondari mji mpya, Maabara ya Shule ya secondari Rau,
madarasa manne Moshi Technical, Majengo ya Hospitali ya Pasua na Sehemu ya
barabara ya Mwamedi Sadiki, inayounganisha kata ya Boma mbuzi na Majengo mapya.
Akitoa maelezo ya barabara hiyo, Mwenyekiti wa
Mtaa, kata ya Majengo Mapya, Beatrice Kimambo alisema kuwa barabara hiyo ambayo
alidai baada ya kuona ujenzi wake haukidhi viwango yeye pamoja na viongozi
wenzake katika ODC walimuuliza diwani wao lakini walijibiwa kwamba swala la
barabara hiyo haliwahusu.
Wanaolalamikia katika ubadhirifu wa ujenzi wa
mifereji katika barabara hilo ni Meya wa Moshi ambaye ndiye diwani wa kata ya
Boma mbuzi, Japhary Michael na Diwani wa Majengo Mapya, Charles Makarakara.
Kimambo aliwaeleza viongozi hao kwamba katika
kufuatilia gharama zilizotumika katika ujenzi wa kingo za miferuji katika
barabara hiyo ambayo mwaka mmoja tuu tangu ijengwe imeanza kubomoka, waliambiwa
na diwani wao kuwa ni bilioni moja.
0 comments:
Post a Comment