SERIKALI ya Tanzania imeomba Malawi iache
kutapatapa kuhusu mgogoro wa mipaka wa ziwa Nyasa kufuatia Rais wa nchi
hiyo, Joyce Banda kutangaza katika baadhi ya vyombo vya
habari kuwa atapeleka suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya
Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la usuluhishi lifanye kazi na
litoe maamuzi.
Aidha serikali imesema kuwa hata
siku moja haijapelekewa taarifa wala nyaraka za siri kutoka kwa Katibu wa
jopo hilo, ambalo linahusisha marais wastaafu wa zamani wa Afrika na
wanasheria kama ilivyodaiwa na Rais Banda katika vyombo
hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk. John Tesha ambaye wanaamini
ametoa habari na kuiba nyaraka za siri.
Akilitolea ufafanuzi jambo hili,
Waziri Membe amesema kuwa Tanzania na jopo hilo
limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais Banda kupoteza
imani.
Kwa kuwa baada ya kuwasilisha barua na nyaraka
zake Dk. Tesha hatahusika katika suala hilo ili kuondoa uwezekano wa nchi
hiyo (wenzetu) kulalamika. Pia hata marais wastaaafu kutoka
katika nchi zenye migogoro ya mipaka hawatahusika kwa sababu
ya kuzuia ‘confilict of interest’.
“ Serikali ya Tanzania ina imani na
jopo linaloongizwa na Rais mstaafu wa Msumbiji , Joachim Chissano na marais wengine
ambao ni Festus Mogae na Thabo Mbeki , kwa kuwa lina watu wenye
uzoefu, wataalamu na wachapakazi. Pia kuna jopo la wanasheria
na wataalamu wa masuala ya migogoro limeundwa na ni la
watu saba,” alisisitiza Waziri Membe.
Aliwataja wanasheria hao kuwa
ni Jaji Raymond Ranjeva, ambaye ni Jaji mstaafu wa ICJ, Profesa George
Kanyeihamba(Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Uganda, Jaji Baney Afako (Mshauri
wa masuala ya sheria kwenye Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa mpaka wa Sudan),
Dk. Gbanga Oduntun(Profesa wa Sheria na Mjumbe wa Kamisheni ya
mgogoro wa mpaka kati ya Nigeria na Cameroon).
Wengine ni Profesa Martin Pratt,
(ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Geografia na Mipaka), Dk. Dire David Tladi
(Mjumbe wa Kamisheni ya Sheria ya Umoja wa Mataifa) na Miguel
Chisano(Kiongozi wa Chuo kinachoshughulikia mipaka ya Baharini na Nchi
Kavu.
“ Ni watu wenye heshima ya dunia
tusingetegemea--- kusema hana imani na jopo hili,” alisema.
Akirejea mazungumzo ya makubaliano
yaliyofanyika Novemba 17, mwaka jana(2012) kuwa walikubaliana hapo walipo
katika jopo hilo ndipo sehemu ya mwisho. Hivyo wataenda ICJ iwapo watashauriwa
na jopo la mzee Chissano.
‘’Wakati tunasubiri jopo kufanya
kazi na kutoa majibu serikali inaiomba Malawi pale katikati ya Ziwa Nyasa
pasiguswe mpaka jibu litakapotolewa na jopo la usuluhishi. Tunaiomba serikali
ya Malawi irudi katika jopo la usuluhishi na tutashangaa ikiwa
Malawi itakwenda kushtaki ICJ kwa kuwa ili Malawi iende
ICJ ni lazima sisi tukubali. Hata pale tutakaposhauriwa ni
lazima sisi tukubaliane na Malawi,” alisisitiza Waziri Membe.
Hivyo aliiomba serikali ya
Malawi iache kutapatapa mara Uingereza, Marekani ,Jumuia ya Madola na
Umoja wa Afrika(AU) na kuona viongozi mbalimbali wa dunia, bali iamini jopo la
Mzee Chissano. Matokeo ya utafiti wao upo uwezekano wa kuyakubali au
kuyakataa.
Akizungumzia kuhusu utoaji wa ripoti ya
jopo hilo utakuwa ni lini,Waziri Membe alisema Tanzania haina haraka juu ya
jambo hilo.
Waziri Membe alisema Tanzania ,
ilipeleka wataalamu Uingereza na Ujerumani ili kupata uelewa wa kutosha
juu ya jambo hilo, hivyo ina ushahidi wa kutosha.
0 comments:
Post a Comment