SERIKALI imepunguza
gharama za chanjo na dawa za mifugo kutokana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Uzalishaji
Chanjo za Mifugo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Profesa
Uswege Minga katika uzinduzi wa maadhimisho wa siku ya Veterinari dunia
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Chanjo zinazozalishwa
katika taasisi hiyo ni chanjo ya Mdondo (Newcastle disease Vaccine), chanjo ya
Kimeta (Anthrax disease Vaccine),chanjo ya Chambavu(Blackquater disease
vaccine) na chanjo ya mtupaji mimba
(Brucella Abortus Vaccine).
Alisema kuwa awali
Tanzania ilikuwa inaagiza dawa na chanjo hizo kutoka nje ya nchi ambapo ilikuwa
inatumia fedha nyingi za kigeni kupata chanjo hizo ambazo hata hivyo zilikuwa
hazikidhi mahitaji.
Serikali kupitia Wizara
ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ilianzisha taasisi hiyo chini ya TVLA ili
kuwezesha upatikanaji wa chanjo kwa wakati na kuepuka matatizo yaliyokuwa
yanajitokeza kutokana na kuagiza chanjo kutoka nje ya nchi.
Profesa Minga aliongeza
kuwa upatikanaji wa chanjo hizo pia umewezesha uchanjaji wa mifugo kwa njia ya kampeni
kwa urahisi zaidi kutokana na chanjo hizo kukidhi mahitaji yaliyokusudiwa.
“Kupatikana kwa chanjo
hizo pia kumefanikisha kumefanikisha kampeni za uchanjaji katika maeneo yote na
kudhibiti ugonjwa uliokusudiwa,kwasababu hiyo magonjwa mengi ya milipuko
yamedhibitiwa kuenea hapa nchini”, alisema mwenyekiti huyo.
Maadhimisho ya
Veterinari duniani ufanyika kila mwaka mwezi Aprili ambapo wataalam wa mifugo
duniani kote hutoa huduma mbalimbali za mifugo ikiwemo chanjo,elimu kwa
wafugaji na wadau wengine na maonesho ya mazao ya mifugo.
Kauli mbiu ya
maadhimisho ya mwaka huu ni “Chanja ili kuzuia na kulinda” na kilele cha
maadhimisho hayo ni Aprili 27, mwaka huu, ambapo wataalam wanahimizwa na
kuhamasishwa kutekeleza mikakati na mipango ya kitaifa na kimataifa.
0 comments:
Post a Comment