Timu
nne zitakazochuana katika kipindi cha tatu cha Guinness Football Challenge wiki
hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu,
Uganda- kijani na nyeusi ni timu kutoka Kenya.
Meneja
wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(kulia) na mtangazaji wa kipindi cha
Tamasha la michezo Amry Masare wakijadili na kufanya uchambuzi wa kipindi cha
kwanza na pili cha Guinness Football Challenge jana katika kipindi cha Tamasha
la michezo kinachorushwa na televisheni ya ITV.
********** *********
Francis
na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya
Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha
mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV,
timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka
mshindi na kutambulika kama wachezaji na
si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano
ya Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa
ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi
kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15)
usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku
.
Katika
Episodi ya tatu ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya
ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi
itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote
yatapatikana siku ya Jumatano.
Hizi
ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.
Timu
ya bluu-Tanzania:
·
Mohamed Kobembe na Gullam
Sosha wenye umri wa miaka 23 kutoka Dar es
Salaam watashirikiana kuona kama wataweza kushinda katika kipindi cha tatu cha
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.Mohamed ndiye kichwa cha timu ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya maswala ya kodi na Gullam
ambaye ni mchezaji wa Ndanda FC, wana matarajio ya kufanya vizuri katika mashindano
hayo.
Timu
nyekundu-Kenya:
·
Kenneth Kamau mwalimu wa
timu ya vijana(23) na Willis Ogutu(miaka 30) wote kutoka Nairobi watachezea
Kenya.Keneth ataonesha maarifa yake ya soka wakati Willis ataonesha uwezo wake wa kucheza
mpira.
Timu ya kijani-Uganda:
·
Kennedy Mwota(22) kutoka
Naijanakumbi na Steven Nsubuga(25) kutoka Kampala.Kennedy ni mwanafunzi na
Steven ni muhasibu.Kennedy ataonesha ujuzi wa soka na steven kipaji chake cha kusakata kabumbu.
Timu nyeusi-Kenya:
·
Wafanya biashara wa
Nakuru,Stephen Kaguda,35 na Gideon Onyango,34, watavaa jezi meusi. Stephen
ambaye ni mshabiki wa Barcelona FC atakuwa akijibu maswali wakati Gideon ambaye
ni mshabiki wa Man Utd atachezea mpira.
Wapenzi wa kipindi hiki
cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza
kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.
Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili
bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya,
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari
zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia
na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya
bia uipendayo ya Guiness wakati
unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa
walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.
Tafadhali Kunywa kistarabu.
0 comments:
Post a Comment