Wakati
umewadia tena wa kushuhudia mapambano katika kipindi ukipendacho cha
Televisheni na kinachotambulika kama, “The
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™”, ambacho kinarudi kwenye runinga yako wiki hiii tarehe 20 mwezi huu wa tatu.
Mwaka huu
watazamaji watapata nafasi ya kuangalia mchuano huu wa kipindi hiki katika
televisheni mbili ikiwemo televisheni ya
ITV na Clouds TV ambazo zitarusha kipindi hiki kwa muda tofauti tofauti siku
hiyo ya Jumatano.
Ikumbukwe
kwamba mamia ya vijana kutoka kona mbali
mbali nchini walichuana vikali hapo leaders
club ambapo walikua na nafasi ya kuweza kuingia kwenye shindano ambalo
lingewawezesha kujishidia kitita cha dola za kimarekani $250,000.
ipindi hiki cha televisheni kinachotazamwa
na wengi barani Afrika kimerudi tena kwa kishindo na kwa sasa kitakuwa
kinashirikisha nchi za barani Africa. Washiriki watakuwa kutoka nchi za Cameroun,
Ghana, Kenya, Tanzania and Uganda na washindi wa mwisho kabisa watajipatia tuzo
ya ‘Pan-African champions.’
Washiriki
wote watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kwamba wanaweza
kuwakilisha nchi zao ipasavyo . GUINNESS ilipigania kutafuta kwa hali ya juu washiriki
walio na uwezo mkubwa na waliokuwa tayari kuonyesha vipaji vyao na ujasiri
kwenye mchezo wa soka. Timu zote zitashiriki
kwa vipaji na kwa uelewa wa soka yaani kwa kiingereza, ‘Skill and Knowledge’ . Kwa hivyo kila timu ina washiriki
wawili. Mmoja kwa maswala ya uelewa na
mwingine kwa suala zima la kipaji.
Kwa kuanza
kabisa, watanzania waliofuzu kusafiri watakutanishwa wenyewe kwa wenyewe
jukwaani, na kupewa maswali na nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye
soka. Baada ya hapo watakaothibitisha kuwa
wapo juu zaidi kwa asilimia mia, watapata nafasi ya kuingia kwenye shindano
lenyewe wakipewa dhamana ya kubeba bendera ya nchi yao. Wengine watarudi
nyumbani.
Usikose
kipindi cha kwanza kabisa ambacho kitarushwa hewani na televisheni ya ITV saa
tatu na dakika kumi na tano usiku na Clouds TV
saa mbili na dakika kumi na tano usiku siku ya jumatano
tarehe 20 machi mwaka huu. Katika
kipindi hiki, tutapata nafasi ya kushuhudia timu yetu ikichuana vikali katika raundi ya kwanza.
Timu kwenye raundi ya kwanza :
Timu ya bluu –
Tanzania:
Kutoka Dar es
Salaam, Daniel Msekwa, ndiye kiongozi
kwenye maswala ya maswali yanayohusiana na soka, Mwalimu Akida Hamad, naye ataonyesha kipaji
kwa kucheza . Daniel ni mfanyakazi wa
shirika la bandari Tanzania yaani TPA na Mwalimu bado ni mwanafunzi wa chuo cha
elimu ya juu. Wote wanakubali kwamba
mchezo huu umewapa nafasi vijana wengi kuonyesha vipaji vyao na kwamba unainua
soka sio kwa kucheza tu bali na kuwa na uelewa kuhusu mchezo mwenyewe. Je wataweza kuendelea kwenye hatua ya pili?
Timu Nyekundu
– Kenya:
Hawa wapenzi
wa michezo mmoja ni Michael Kirwa, na mwenzake ni mwalimu wa mazoezi yaani ‘fitness trainer’ Stephen Githinji, wote
wa jiji la Nairobi. Michael yupo hapa
kwa maswala ya kujibu maswali yani uelewa wa soka naye Stephen ndiye
atakayeonyesha vipaji kwa kucheza.
Timu ya
kijani – Uganda:
Oscar Boban na
Kennedy Andindu, wanatokea kampala na
ndio watakaoakilisha Uganda katika hiki kipindi cha kwanza. Oscar ni mfanyabiashara na ndiye atakayekuwa
mshiriki wa uelewa na kennedy ambaye ni mpenzi wa Arsenal .Yeye atakuwa jukwaani
kuonyesha kipaji chake.
Timu Nyeusi –
Kenya:
Daniel
Muthendu, ni mhasibu na amekili ni
mpenzi mkubwa wa soka na kujiamini kuchuana kwenye maswali yote yanayohusu mpira
huu wa miguu. Mwenzake ni Oscar Litonde, ambaye ni mchezaji wa mpira, mechi za kirafiki
jijini Nairobi. Hawa nao pia watachuana
vikali na timu tajwa hapo juu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football
challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa
kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya
hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika
tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu
ya mkononi na kompyuta zao.
Pia GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook page www.facebook.com/guinnesskenya
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri,
unatakiwa kuupenda ukurasa huu yaani ‘like’ na utakuwa unapata habari zote kama
zinavyotiririka.
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
kimataifa ya Endemol iliyopo Afrika Kusini.
Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako.
Usisahau kuwa
na kinywaji chako ukipendacho cha Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na
nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.
0 comments:
Post a Comment