Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2013


 
 Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-DSM
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, wamerejea jijini Dar es Salaam na kupokelewa kwa shwangwe na mashabiki na wapenzi wa timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Azam waliwasilini kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways ambapo baadhi ya wachezaji wakiwapo wanaoichezea timu ya Tifa Taifa Stars kubaki Naorobi ispokuwa Mcha.

Azam ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara walikuwa Nchini Liberia kuchuana na timu ya  Barrack Young Controllers (BYC) ambapo Azam walishinda 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.

Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, Raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.


 Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo.


Baadhi ya Mashabiki na Wapenzi wa Timu ya Azam FC wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa Mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.

SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.

Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao
Posted by MROKI On Tuesday, March 19, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo