Mahmoud
Ahmad Arusha
Wakazi wa
jiji la Arusha leo wameonja joto ya jiwe na adha ya mgomo wa usafiri wa dala
dala ukihusishwa na masuala ya rushwa na kisiasa yanayoendelea kwenye jiji hili
huku wananchi wakitembea umbali wa takribani kilometa 6 kwa miguu kufika
katikati ya jiji hili.
Mgomo huo
ulioanza tangia Alfajiri hadi saa tisa mchana uliacha shughuli za kimaendeleo
kusuasua kwa muda huku wakazi wa maeneo ya Mbauda,ffu,kwa Morombo,na kisongo
wakionja joto ya jiwe kutokana na mgomo huo.
Suala la
rushwa kwa askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na suala la
kisiasa yamehusishwa moja kwa moja na mgomo huo ambapo baadhi ya madereva na
makondakta waliohojiwa na wanahabari wamesema kuwa askari wamakuwa wakiwatuma
chips kuku kila wanapowakamata.
Madai hayo
yalienda sambamba na madai yaliyotolewa yakimuhusu mwanasiasa moja jijini hapa
kuwahamasisha madereva hao kugoma kwa masuala yake ya kisiasa na huku madereva
hao wakilaumu jeshi la polisi kuwakamata kwa siku hadi mara tano hali inayoleta
usumbufu kwa madereva hao kukosa posho zao za kila siku
“utakuita
trafiki anakutuma chips kuku na saingine anakwambia utupie buku jero huku ni
kuumizana kwani inakuwa tunawafanyi kazi wao na familia zao huku tukitoa
malalamiko yetu kwa mkubwa wao yamekuwa yakiishia hewani sasa leo tumeamua
kugoma”alisema moja wa madereva hao wa mbauda
Akizungumza
na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela alisema kuwa hakuna
aliyejuu ya sheria na kuwa yeyote atakayebainika kuchochea vurugu hizo
zilizoenda sanjari na mgomo hatua kali za kisheria zitafuata mkondo wake na
kuwa hawatafumbia macho wale wote wanaotumia makundi kuwathiri wananchi kwa
manufaa yao ya kutaka umaarufu.
Alisema
kuwa wameunda kamati ya muda kutatua masuala yote ya usafiri wa daladala
almaarufu Vifodi jijini hapa na kuwa hawatangoja hadi mgomo utokee tena kwani
kila mwezi watakuwa wakikutana kupeana taarifa na matukio mbali mbali iliwaweze
kuyatatua kwa wakati.
“unajua
mgomo huu usitumiwe na wanasiasa kutaka kujipatia umaarufu kwani wamakuwa
wakiwashaiwishi vijana kufanya matendo ya siyo ya kiustaarabu anaakibainika
mwanasiasa yeyote kuwa waliwashawishi vijana kuwazuia madereva kuendesha mgomo
huo hatutasita kuchuwa hatua kali za kisheria dhidi yake hatutamuogopa mtu
kwenye hili”alisema Mongela
Mgomo wa
vifodi jijini hapa umekuwa ukihusishwa na mambo ya kisiasa kwa kila mara jeshi
la polis mkoani hapa linapozuia maandamano ya chama kimoja cha siasa wamekuwa
wakitumia vijana kuwadhibiti madereva wa vifodi kutoendesha kazi zao huku
wakitoa vitisho na saa ingine kuwapiga madereva wanaokaidi amri yao
Wananchi
kadhaa waliohojiwa wameitupia lawama za moja kwa moja mamlaka husika kwa
kufumbia macho vitendo vya vijana hao waliokuwa wakizuia magari kuingia jijini
hapa kwa madai kuwa wametumwa kutoka ngazi za juu.
0 comments:
Post a Comment