Evelyn
Mkokoi,Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira dkt Terezya Huvisa, amezingua moja ya
miradi wa maji safi na salama, katika kijiji cha Ng’mbo wilaya mpya ya Nyasa
katika mkoa wa Ruvuma ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na athari
zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Akizindua
kisima hicho, Dkt Hufisa alieleza kuwa, mradi huo wa maji safi na salama kwa
matumizi ya binadamu katika kijiji hicho umewalenga zaidi wanawake kwani wao
wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kutafuta maji ziwani au katika visima vya
muda kwa matumizi ya nyumbani,hivyo kisima hicho kitawasaidi kuokoa muda na
kushiriki katika shughuli nyingine za kimaendeleo.
Dkt
Hufisa aliongeza kwa kusema kuwa, wananchi wana haja na kila sababu ya kupata
elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira, na
halmashauri iweke mikakati ya kutunza vyanzo vya maji pamoja na kupanda miti na
kuitunza.
Aidha
dkt Huvisa amewaasa wananchi kushirikiana na police jamii wanaosimamia masuala
ya mazingira katika kubaini waharibifu wa mazingira wanaovua kwa kutumia nyavu
na uvuvi haramu.
Awali mratibu wa kitaifa wa mradi huo kutoka Ofisi
ya Makamu wa Rais Mazingira bw. Faraja Ngeregeza ameeleza kuwa, lengo la mradi
huo ni kujengea uwezo wananchi na wanakijiji ili kuweza kuhimili athari
zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi hasa zinazotokana na upungufu wa maji
safi na salama.
Bw.
Faraja alisema kuwa kijiji cha Ng’ombo hakikuwa na maji safi na salama kwa muda
mrefu hali iliyowalazimu wanakijiji hichohususan kina mama kutembea muda mrefu
kutafuta maji kwa matumizi ya nyumbani. “kukamilika kwa mradi huu kumetoa fursa
kwa kina mama kupata maji kwa muda mfupi na kupata muda wa kushiriki katika
shughuli nyinine za kimaendele.”alisisitiza.
Mradi
huu unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira unafadhiliwa na serikali
ya japan kupitia shirika la maendeleleo la umoja wa mataifa unatarajia
kukamilisha ujenzi wa visima vingine katika wilaya ya misenyi mkoani
Kagera,Igunga mkoani Tabora na maeneo ya Nungwi mjini Zanzibar ikiwa ni kwa
ajili ya kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
0 comments:
Post a Comment