TAMASHA la
Muziki la Sautio za Busara ambalo linafanyika kila Mwaka Visiwani Zanzibar
katika viwanja vua Mji Mkongwe limetajwa kuwa ni ni miongoni mwa Matamasha kumi
bora ya Muziki barani Afrika.
Tamasha
hilo ambalo sasa nila miaka takribani 10 tangu kuanza kwake limekuwa
likukusanyahi mbalimbali pamoja naa maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali
duniani na kulifanya kunyakua nafasi ya nane ya Matamaha hayo kumi bora Afrika.
Sauti za
Busara ni Tamasha ambalo hutawaliwa na matukio mengi ya burudani za muziki wa
asili (Ngoma) ambapo zaidi ya wasanii 200 hushiriki na kuonesha kazi zao
mbalimbali za kimuziki.
Pia katika
siku za tamasha hilo huwepo mbio za majahazi na burudani nyionginezo nyingi.
Katika
Mlolongo huo Tamasha la Muziki la Asabaako
kutoka Nchini Ghana ambalo hufanyika kila mwaka katika fukwe ya Busina ndio
limeshika nafasi ya kwanza.
Asabaako ni tamasha ambalo
huwaleta pamoja ma DJ’s kutoka Ghana, Amerika na Ulaya huku miondoko ya Azonto
kipasua anga kwa njia za mitandao ya kijamii ya Youtube hadi ulaya kunako
miondoko ya Afrotronica na mwisho wa Tamasha hilo kunaangushwa bonge la Bush
Party.
Nchi ya Moroco inashika
nafasi ya pili katika Ukali wa matamasha bora Afrika kufuatia Tamasha lake la FDE
ambalo hufanyika kila mwaka kwa miaka 15 sasa kaytika mji wa Essaouira na
kuwavuta zaidi ya wasanii 30 wa ndani na nje na hujulikana kama “Morocco’s answer to Woodstock”,
Nafasi ya
tatu ina kwenda kwa Tamasha la sur le
Niger ambalo si kuwa linafanyika Nchini Niger pekee bali pia
katika pwani ya Mto Niger katika mji wa Segou nchini Mali.
Katika
Kipindi cha Miaka 9 iliyopita iliwahusisha wakongwe Fela Kuti, King
Mensah, Amadou & Mariam, na Oumou Sangare.
Mawazine
(“Rhythms”) ni moja kati aya matamasha makubwa duniani ya Musiki ambalo
hufanyika kila mwaka na limewahi kuwashirikisha wasanii wakubwa duniani kama Mariah
Carey, Stevie Wonder, Shakira, Whitney Houston, Lenny Kravitz, LMFAO na
Evanescence. Tamasha hili pia hufanyika nchini Morocco. Mshindi wa Tuzo ya
Grammy kwa mara 10, George Benson alitumbiza katika tamasha hilo la 12 mwaka
huu huku kiingilio kikiwa ni bure na kuwavuta zaidi ya watazamaji milioni 1.
Nafasi ya 5 inashikwa na
tamasha la Oppikoppi la nchini Afrika Kusini huku nafasi ya 6
ikienda kwa Tamasha la Kimataifa la Bayimba la nchini Uganda na Kenya wakiingia
katika nafasi ya 7 na tamasha lao la Rift
Valley.
Nafasi ya 9 Desert la nchini
Mali na nafasi ya kumi kwenda nchini Nigeria katika Tamasha lake kubwa la Mziki wa Jazz Lagos ambalo hufanyika Mwezi Novemba kila
mwaka.
Miongoni mwa wasanii
mashuhuri walio tumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Hugh Masekhela, Morrie Louden na Mkali wa miondoko ya jazz Fourplay.
0 comments:
Post a Comment