Nafasi Ya Matangazo

March 17, 2013


Na Mwandishi Wetu

Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa  siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.



Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema jana kuwa utambulisho huo utasindikizwa na burudani kababembe kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.



Kalinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei.



Utambulisho wa Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti 5 na Kitwe General Traders na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.



Mratibu huyo alisema warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.



Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu.



Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Posted by MROKI On Sunday, March 17, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo