Nafasi Ya Matangazo

March 10, 2013

Na Bashir Nkoromo
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro  amesema leo kwamba katika ziara hiyo Kinana atakuwa na msafara wa  watu 14, ambao baadhi yao ni Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM, Makatibu wakuu wa Jumuia za Chama na Wenyeviti wa Chama wa mikoa.

Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, Dk. Asha-Rose alisema, Kinana na msafara wake wanatarajiwa kufika Guangzhou China keshokutwa, Machi 12, 2012.

Alisema, ziara hiyo ambayo ni ya kwanza nje ya nchi kwa Kinana tangu kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM,  Oktoba, mwaka jana,
imeandaliwa na Chama Cha Kimomunisti cha China kwa lengo la kupata fursa ya viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya vyama na wananchi wa nchi Dk. Asha-Rose alisema baada ya kuwasili Guangzhou, kinana na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao wa Chama Cha Kikomunisti
cha China watatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo jiji la Dong-guan, Shenchen, Chengdu, Machi 13-14, 2013, msafara utakwenda jiji la Chengdu, Sichuan, Nanchong na kumalizia ziara hiyo katika jiji la Beijing ambako atawasili Machi 18, 2013.
Tanzania na China zimekuwa na uhusiano wa siku nyingi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni na pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kimkomunisti cha China (PCP) ambavyo ni vikongwe vimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia kwa miama mingi na uhusiani huo uanelezwa kuendelea kukua na kuimarika siku hadi siku.Ushirikiano unaoonekana kuwa wa kindugu wa nchi hizo za Tanzania na China uliasisiwa tangu enzi za waliokuwa viongozi wa nchi hizo,

Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere na  Mao Tse Tung.Moja ya miradi inayotghibitisha uhusiano na urafiki wa kindugu baina ya China ya Tanzania, ni mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya TAZARA  na maradi wa TAZAMA, Mradi wa zana za Kilimo Ubungo,  mradi wa kiwanda cha Mang'ula na wa kiwanda cha nguo cha urafiki.
Posted by MROKI On Sunday, March 10, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo